Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akiiagiza Menejimenti ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuhakikisha inasaidia katika kukuza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvivi, alipofanya ziara katika Benki hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine, akitoa maelezo ya mafanikio ya Benki hiyo, wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Ishmael Kasekwa (Kushoto), akieleza jambo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (kulia) katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji TADB, Bw. Japhet Justine.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Mzee Kilele, akifafanua jambo, wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine, akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (katikati), baadhi ya ofisi za Benki hiyo, alipofanya ziara katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine, akitoa maelezo ya mafanikio ya Benki hiyo, wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Derick Lugemala, akieleza kuhusu unafuu wa riba ambao unatolewa kwa wakopaji, wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Ishmael Kasekwa (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Japhet Justine, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Menejimenti ya Benki ya TADB, jijini Dar es Salaam.
(Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)
**************************
Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuhakikisha inasaidia kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka mitano hususani katika kukuza sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Mhandisi Masauni ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipotembelea Benki ya TADB ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Benki hiyo, katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Masauni alisema kuwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano, sekta ya kilimo ni ya kipaumbele kwa kuwa inaenda kuchochea maendeleo ya viwanda ambavyo vingi vinategemea malighafi ya kilimo, mifugo na uvuvi.
“Nataka Benki hii ipime mafanikio yake katika kuinua mazao ya kimkakati ambayo yameainishwa ikiwa ni pamoja na zao la Kahawa, Chai, Korosho, Pamba, Michikichi, Alizeti na mengineyo, ambayo ni muhimu katika mipango ya Serikali na kukuza uchumi wa nchi”, alieleza Mhandisi Masauni.
Alisema kuwa Benki ya TADB inajukumu la kuhakikisha inasaidia wakulima nchini katika mazao ya kimkakati bali pia kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo na masoko.
Mhandisi Masauni alisema katika sekta ya kilimo yapo maeneo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa ili kuleta tija kwa nchi ikiwa ni pamoja na eneo la umwagiliaji, upatikanaji wa mbegu bora na ugani.
Pia alisema kuwa ni lazima Benki hiyo iibue fursa za maendeleo kwa kushirikisha taasisi zingine, kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Jumuiya za Wafanyabiashara Tanzania, kwa kuwa kuna wanaoweza kuja na fedha za uwekezaji nchini lakini hawazijui fursa zilizopo katika Sekta ya kilimo.
Aidha Mhandisi Masauni ameipongeza Benki hiyo kwa kuwa na maono ya kuwa chombo cha mapinduzi ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na pia kuendelea na kukuza mtaji ambapo wakati wa kuanzishwa kwake Benki hiyo ilikuwa na mtaji wa Shilingi bilioni 50 hadi kufikia bilioni 80 kwa sasa.
Alisema licha ya ukuaji wa mtaji huo bado hautoshelezi katika utekelezaji wa mikakati ya Benki kwa kuwa uhitaji ni takribani Shilingi bilioni 800, hivyo ameitaka Benki hiyo kupeleka mapendekezo yanamna ya kukuza mtaji na Serikali inavoweza kusaidia, ili Benki hiyo iweze kuwa tegemeo katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuchangia uwekezaji katika sekta hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TADB, Bw. Japhet Justine, alisema kuwa mwaka 2018 walitoa mikopo ya Sh. bilioni 33 lakini hadi Julai mwaka 2021 wametoa mikopo za zaidi ya bilioni 340, hivyo kuendelea kutumiza nia ya kuwagusa wananchi kwa nguvu zaidi katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Aidha amemshukuru Naibu Waziri huyo kwa kufanya ziara katika taasisi yake na kuibua changamoto za kuhakikisha wanafungua fursa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuangalia unafuu wa riba ili kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara, na aliahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa.
Hadi sasa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ametembelea Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo takribani 12 Tanzania Bara na Zanzibar.