MSAFARA wa kikosi cha Yanga SC uliopo Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo umetembelea vituo vya kulea watoto Yatima vya Amokachi na Subira Mina Rahman na kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika vituo hivyo.
Yanga SC Jumapili itamenyana na watani wao wa jadi, Simba SC Fainali ya Azam Sports Federation Cup Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.