Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mwembesongo, Abdula Omary akichangia mada wakati wa kongomano la Benki ya NMB na Walimu lililofanyika mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Marthin Shigela (katikati) akizungumza jambo na Meneja Wwandamizi Mikopo kwa Watumishi na Taasisi za Serikali Benki ya NMB, Emmnuel Mahodanga (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma za Kidigitali, Tito Mangesho baada ya Mkuu huyo kufungua kongomano la Bbenki ya NMB na Walimu lililofanyika Mkoani Morogoro.
**************************
Wakuu wa mikoa ya Singida na Morogoro, Dr. Binilith Mahenge na Martin Shigela kwa nyakati tofauti wamekiri kuwa benki ya NMB imekuwa kinara katika kuimarisha waalimu kiuchumi kupitia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.
Wakizungumza katika warsha za siku ya mwalimu ambazo huandaliwa na Benki ya NMB katika mikoa yao, Wakuu hao wamewasisitiza Waalimu kuzitumia vyema huduma za benki hiyo katika kujiimarisha kiuchumi.
Katika warsha ya mkoani Singida, Mkuu wa Mkoa huo, Dr. Mahenge alisema kuwa NMB imekuwa na huduma nzuri zaidi za mikopo ambayo ni rafiki na haina masharti magumu kwa walimu. Hivyo akawasihi waalimu wachangamkie fursa hiyo na akashauri waweze kutumia mikopo hiyo katika kilimo cha alizeti ambayo inastawi sana mkoani hapo huku zao hilo likiwa chanzo kikubwa cha mapato katika mkoa wa Singida.
Dr. Mahenge alitumia fursa hiyo pia kuwasihi waalimu watumie siku hiyo kujifunza mengi kutoka benki ya NMB lakini pia wasiache kushauri na kutoa maoni ya juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo inayohudumia watanzania wengi zaidi.
Akizungumza katika warsha hiyo, Meneja muandamizi wa wateja Maalum wa benki ya NMB Ally Ngingite, alitumia fursa hiyo kuwaomba waalimu wakawe mabalozi wazuri wa huduma za NMB na kuwaasa na wengine kujiunga na benki hiyo kwani ndio benki kinara katika utoaji wa huduma bora na kuwafikia wateja kila mahali.
Kwa upande wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela amekiri kuwa Benki ya NMB imekuwa na mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya watumishi kwani wamekuwa wakisaidia katika utoaji wa mikopo nafuu ambayo kwa wanufaika wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo. Na pia amewasihi ambao bado hawajapata mikopo hiyo wasiache fursa hiyo iwapite kwani ni muhimu sana katika kuwaimarisha kiuchumi.
Aidha, Meneja Mwandamizi wa Mikopo kwa Watumishi na Taasis za Serikali kutoka benki ya NMB, Ndg. Emmanuel Mahodanga alisema Benki ya NMB inaamini katika kutoa huduma za kibenki tena za kidigital kwa watanzania wote ni njia bora zaidi inayoendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na itasaidia kuleta mwamko mkubwa zaidi kwa watanzania wengi
Mahodanga alisema kuwa Benki ya NMB ina wateja zaidi ya 3.2milioni kati yao ni zaidi ya wateja 2.5milioni wanatumia simu kufanya miamala, kuangalia salio, kufanya malipo mbalimbali kama kulipia umeme, maji na hata kulipia kodi mbalimbali kupitia huduma za NMB mkononi.
Siku ya Walimu na NMB hufanyika katika mikoa mbalimbali nchini na kuhudhuriwa na walimu, viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa Sekta ya Elimu.