Manchester United imekamilisha uhamisho wa winga wa kimafaifa wa England, Jadon Sancho kwa ada ya Pauni Milioni 73 kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Sancho mwenye umri wa miaka 21 amesaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na kikosi cha
Ole Gunnar Solskjaer baada ya kufunga jumla ya mabao 54 na kuseti 67 katika mechi 126 Borussia Dortmund aliyojiunga nayo mwaka 2017 akitokea Manchester City ya England pia.
Kwa dau la Pauni Milioni 73, Sancho anakuwa mchezaji wa nne ghali kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo baada ya Harry Maguire (Pauni Milioni 75) Romelu Lukaku (Pauni Milioni 76) na Paul Pogba (Pauni Milioni 94).
Na Sancho anakuwa mchezaji wa pili kulipwa mshahara mkubwa, Pauni 350,000 kwa wiki baada ya kipa, David De Gea anayelipwa Pauni 375,000 kwa wiki.