Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Wazee,Jinsia na Watoto Dkt.Omar Dadi Shajak akizungumza na ugeni wa madaktari bingwa wa upasuaji kutoka nchini Saudia Rabia walipofika kujitambulisha kwa lengo la kuwafanyia upasuaji wananchi wa Kisiwa cha Pemba.
Kiongozi wa madaktari bingwa wa upasuaji kutoka nchini Saudia Rabia Dkt.Yussuf Al-alawi akimueleza Dkt Shajak namna watakavyotoa huduma ya upasuaji.
Picha na Rahima Mohamed
******************************
Ali Issa Maelezo 23/7/2021.
Jopo la Madaktari bingwa wa kutoa huduma za matibabu ya upasuaji na maradhi mengine mbalimbali, kutoka nchini Saudia Rabia limewasili Zanzibar kwa kuwapatia huduma za matibabu wananchi wa kisiwa cha Pemba kuazia kesho.
Akitoa taarifa kwa wandishi wahabari mbele ya madaktari hao waliowasili ofisini kwake Mnazi Mmoja, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee,Jinsia na Watoto Katibu Mkuu Wizara hiyo, Dkt.Omar Dadi Shajak amesema, madaktari hao wata fanya upasuaji kwa wagonjwa mbalimbali ikiwemo uperesheni wa hania.
Alieleza kuwa madaktari hao watakuwepo kwa muda wa siku tano hivyo amewataka wananchi waitumie vyema fursa hiyo kwa maslahi ya afya zao.
Nae kiongozi wa msafara wa madaktari hao Dkt.Yussuf Al alawi alimueleza Dkt Shajak kwamba, wamekuja kutoa huduma hiyo muhimu kwa wananchi na wataanzia katika kisiwa cha Pemba.
Aidha alisema wataisadia hospitali ya Wete kwa kuipatia vifaa vya upasuaji wa maradhi ya mifupa ili kuondoa usumbufu wa kufata huduma izo Unguja.