……………………………………………………………..
Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mhe, Innocent Lugha Bashungwa ameteua Kamati ya kuratibu maandalizi na mashindano ya Tamasha la Michezo ya Wanawake linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hassan Abbasi imefafanua kuwa, kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Bi. Neema Msitha ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na wajumbe 14
Wajumbe 14 wa Kamati hiyo ni kama wanavyoonekana hapa chini:
- Bi. Irene Mwasanga. Kamati ya Olimpiki Tanzania
- Bi. Nasra Mohamed. Idara ya Uhamiaji, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 3. Bi. Nasriya Nassor. Wizara ya Habari, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 4. Bi. Leah Kihimbi. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 5. Bi. Christina Luambano. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 6. Bi. Lilian Nyinge. Ofisi ya Rais, TAMISEMI
- Dkt. Devotha Marwa. Chama cha Mpira wa Pete (Netboli) Tanzania 8. Bi. Amina Karume. Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake 9. Bi. Beatrice Singano. Kampuni ya Airtel
- Bi. Rehema Mwendo. Clouds Media Group
- Bi. Neema Singo. Benki ya NBC
- Bi. Tuli Mwambape. Benki ya CRDB
- Bi. Asha Baraka. Mdau wa Michezo
- Bi Suma Mwaitenda. Mdau wa Michezo
Aidha, Waziri Bashungwa amesema uteuzi huo umezingatia uzoefu kwenye masuala ya michezo na kuandaa matukio (Festival events).