Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ,akizungumza wakati wa uzinduzi Mpango wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki ya Mwalimu (MCB) hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu (MCB) ,Richard Makungwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki hiyo hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Naibu katibu Mkuu wa chama cha walimu (CWT) Japhet Maganga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki ya Mwalimu (MCB) hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi Mpango wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki ya Mwalimu (MCB) hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa Mikopo ya Mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki ya Mwalimu (MCB) hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akikata keki kuadhimisha miaka mitano kuanzishwa kwa Benki ya Mwalimu (MCB) hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu (MCB) ,Richard Makungwa wakati akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza kuzindua Mpango wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki hiyo hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua Mpango wa Mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki ya Mwalimu (MCB) hafla iliyofanyika leo Julai 22,2021 jijini Dodoma.
…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameitaka benki ya Mwalimu (MCB) kuwasaidia walimu nchini mikopo yenye masharti nafuu ili kuondokana na mikopo umiza.
Hayo ameyasema leo Julai 22,2021 jijini Dodoma wakati akizindua mpango wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali ujulikano kama Mwalimu na Ujasiriamali unaoratibiwa na Benki hiyo.
Mtaka amesema kuwa walimu wengi nchini wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu kutokana na aina ya mikopo wanayokopa kutoka katika taasisi ambazo zina masharti magumu na riba kubwa.
Mtaka ameseme kitendo cha kukopa kabla mtu hajapata elimu ya nini anakwenda kufanya kimekuwa chanzo cha wengi kuharibikiwa na kujikuta wanaishi na Madeni yasiyokwisha.
“Kwa hiyo kabla ya kukopesha lazima kwanza muwape elimu wahusika ili kuwapunguzia msongo wa mawazo walimu wetu,” amesema Mtaka.
Aidha amesisitiza kuwa ifike hatua benki ya Mwalimu mtazame vipi mnakuja kwa utofauti gani na taasisi nyingine za kifedha ili muweze kuwakopesha walimu wenye uhitaji fedha kwa ajili ya kufanya mambo mbalimbali yanayo wakabili bila kuwapatia usumbufu wowote.
Hata hivyo ameitaka benki hiyo kuwa na mkakati mzuri wa kiushindani na mabenki mengine ili wajipambanue kama kimbilio la wanyonge.
“Hili jina la Mwalimu benki mnaweza kuendelea nalo lakini lazima muone kuwa utendaji wenu uwe kwa ajili ya makundi yote ili muweze kushindana na benki nyingine zaidi ya 50, zilizopo nchini”amesisitiza
Hata hivyo ameeleza kuwa benki hiyo inatakiwa kujikita katika kuhakikisha kuwa inakuwa na kitu cha utofauti ambacho kitawavutia walimu na kujiunga nayo.
Pia amesema kuwa mpango huo wa mikopo ya mashine za uzalishaji mali amesema kuwa ni ubunifu mzuri ambao kama utasimamiwa vizuri utawawezesha walimu kustaafu wakiwa na tabasamu.
Hata hivyo amewataka walimu nchini kuchangamkia mkopo huo wa vifaa ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Mtaka amewataka walimu kutokimbilia mijini wakishastaafu kwani wanajiongezea matumizi bila sababu za msingi kwa vitu ambavyo wangeweza kuviepuka.
Pia amewaagiza walimu mkoa wa Dodoma kufundisha kwa bidii,juhudi na maarifa yote kwani mkoa bado unawahitaji na Taifa linawategemea zaidi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu (MCB) ,Richard Makungwa amesema katika jitihada za kuunga mkono Serikali kwenye kukuza sekta ya viwanda na biashara mwalimu Benki imeanzisha bidhaa mpya ya mwalimu na ujasiriamali.
Amesema bidhaa hizo zitawawezesha walimu,watumishi wa Serikali pamoja na umma kuweza kukuza na kuwajengea uwezo kupitia shughuli za ujasiriamali ili kuwakwamua kiuchumi.
Amesema mwalimu benki kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watatoa mikopo ya mashine mbalimbali za ujasiriamali zitakazowawezesha walimu waliopo kazini kuweza kujitengenezea kipato cha ziada na wale waliokaribia kustaafu kuweza kujiandaa na maisha ya ujasiriamali ili wanapostaafu wawe na biashara ambazo tayari wana ujuzi.
“Mashine hizi zimezingatia teknolojia gharama na ufanisi ambazo pia zitakatiwa bima na watumiaji watapewa mafunzo na kufungiwa kabisa mashine sehemu za uzalishaji,”amesema.
Amesema mashine hizo zinapatikana kwa bei ya shilingi milioni 5 hadi 15 ambapo amedai zipo za aina mbalimbali ambazo ni za kutengeneza sabuni,kusaga nafaka,kubangua korosho,kutengeneza siagi,kukausha na kusaga viungo mbalimbali vya chakula.
Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema Mwalimu Commercial Bank iliandaa mkakati wa muda mrefu ukiwa na malengo ya kuboresha huduma zenye ubunifu na ufanisi katika kuwafikia wateja.
Amesema maeneo waliyoyapa kipaumbele ni pamoja na kuwa na bidhaa zinazolenga moja kwa moja mahitaji ya walimu katika kujiinua kiuchumi na kuleta tija katika jamii.
Vilevile,amesema benki hiyo imelenga utoaji wa huduma za kibenki ambazo ni rahisi,salama na zinazopatikana popote na wakati wowote kwa njia ya Kidigital ili kuwafikia wateja zaidi ya 43,000 pamoja na wateja watarajiwa ambao ni walimu pia wanahisa zaidi ya 200,000 waliosambaa katika Mikoa ya Tanzania.
Amesema benki hiyo ina matawi wawili yaliyopo Dar es salaam na wanazo Ofisi 5 katika Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mwanza,Dodoma na Arusha ambapo amedai kufikia Desemba mwaka huu wanategemea wawe wamefika katika Kanda ya Kusini na Magharibi.
Naye Naibu katibu Mkuu wa chama cha walimu (CWT) Japhet Maganga amesema kuwa wao kama walimu na watumishi wengine wapo tayari kutoa uahirikiano katika kuhakikisha kwamba benki hiyo inaleta manufaa chanya kwa walimu na hata jamii nzima kwa ukubwa wake.