Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akimkabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen.
****
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz ‘Sauti ya Dhahabu’ kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Leseni hiyo ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio na Kanuni za Utangazaji imekabidhiwa leo Alhamis Julai 22, 2021 na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mhandisi Mihayo amesema Leseni hiyo ni ngao ya Gold Fm kufanya kazi huku akiwasihi viongozi wa Gold Fm, kila wanapoamka warejee kwenye kanuni za utangazaji.
“Nawapongeza Gold Fm, haikuwa kazi rahisi, mmepitia michakato mbalimbali, na ndoto yenu leo inatimia baada ya kuwapa leseni. Meneja amejipambanua akisema kituo kitakuwa karibu zaidi na wananchi kuelimisha na kuhabarisha wananchi. Nisingependa kuona Gold fm mnafanya makosa kwa kutofuata kanuni za utangazaji”,amesema Mhandisi Mihayo.
Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa ameitaka Gold Fm kuwa ya mfano kwa kutumia lugha fasaha na yenye staha kwenye matangazo yao akiwakumbusha kutojiachia kwani kuna vipindi vinatakiwa visikilizwe muda flani na vingine havitakiwi.
“Leseni yenu inasema mtatumia lugha ya Kiswahili kufanya matangazo, natumaini kuwa mtatumia Kiswahili Fasaha.Hakikisheni mnafuata ratiba ya vipindi vyenu, kama kuna mabadiliko ya vipindi tupeni taarifa TCRA, Msibadilishe vipindi bila kutoa taarifa TCRA”,ameeleza Mhandisi Mihayo.
Mhandisi Mihayo amefafanua kuwa kuanzishwa kwa Gold Fm kunaifanya Kanda ya Ziwa kuwa na idadi ya redio ya 42 kwa upande wa wilaya ya Kahama kuwa na Redio 4 na mkoa wa Shinyanga kuwa na Redio 5.
Ameongeza kuwa katika mkoa wa Shinyanga kuna redio ipo kwenye mchakato wa kuanzishwa huku akiweka wazi kuwa katika Kanda ya Ziwa bado kuna masafa ya uanzishwaji wa redio hivyo wanaohitaji kuanzisha redio wawasiliane na TCRA ili wapatiwe utaratibu.
Akipokea Leseni ya Utangazaji, Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen amesema wamedhamiria kuleta mapinduzi ya vyombo vya habari Kanda ya Ziwa akibainisha kuwa wanatamani kuwa mfano wa vyombo vya habari vingine kwa kutoa habari zenye usawa bila kupendelea upande wowote.
“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Gold Fm ni kuelimisha jamii,kuhabarisha, kuburudisha, kuchangia uchumi kwa kuhamasisha ulipaji wa kodi za serikali, kuhamasisha amani kwa taifa letu pamoja na kukumbusha wananchi kanuni,sheria na taratibu za nchi”,amesema Neema.
“Nitumie nafasi kuwatambulisha kwenu rasmi kituo kipya cha Redio katika Manispaa ya Kahama, Gold Fm, labda katika siku za hivi karibuni mlisikia uanzishwaji wa kituo kipya cha Redio lakini hamkuwa na taarifa za undani zaidi kuhusu Gold Fm.
Mchakato wa kuanzisha Redio hii ulianza takribani miaka mitatu iliyopita na sasa ni rasmi Gold Fm inasikika hewani kupitia masafa ya 88.7 Mhz”,amesema Neema.
“Ujio wetu huu wa kishindo wa Gold Fm ‘Sauti ya dhahabu’tukitumia kauli mbiu ya Baba Kaingia Mjini, Mdundo unasikika, burudani iendelee tunaamini kabisa jamii itanufaika vya kutosha na wenye matangao tunawakaribisha wote kuja kutangaza kupitia kituo chetu cha matangazo”,ameongeza Neema.
Meneja wa Redio Gold Fm, Faraji Mfinanga amesema kibali chao ni kusikika ndani ya mkoa mmoja ambao ni Shinyanga.
Mfinanga ameyataja baadhi ya maeneo ambako sasa Gold Fm inasikika kuwa ni Manispaa ya Kahama, Ushetu, Msalala, Shinyanga vijijini na mikoa ya jirani ikiwemo Geita wilaya ya Bukombe, Mbogwe na kwa upande wa Tabora, Nzega ,Kaliua na Urambo pamoja na maeneo mengine yaliyo jirani na Kahama ikiwemo wilaya ya Biharamulo na Ngara mkoani Kagera.
Naye Mkuu wa Maudhui na Uzalishaji wa Vipindi Bakari Khalid amewahakikishia wasikilizaji wa vipindi kuwa Gold Fm ni ya kipekee sana kwani wamejipanga kikamilifu kuihabarisha jamii na kutatua matatizo ya wananchi huku akibainisha kuwa watadumisha na kuimarisha ushirikiano na waandishi wa habari na media zingine.
ANGALIA PICHA
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akimkabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen (kulia) leo Alhamis Julai 22,2021 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi leseni iliyofanyika katika Hoteli ya Submarine Mjini Kahama. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akimkabidhi Kanuni za Utangazaji wa Vipindi vya Redio Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen (kulia).
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilichopo Mjini Kahama.
Mkuu wa Maudhui na Uzalishaji wa Vipindi Gold Fm, Bakari Khalid akizungumza wakati Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akikabidhi Leseni ya Utangazaji wa Vipindi vya Redio kwa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, kilicho Mjini Kahama.
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen (kushoto).
Watangazaji wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, iliyopo Mjini Kahama wakiwa ukumbini
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi. Neema Mghen akifuatiwa na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo na Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm Faraji Mfinanga akiteta jambo na (kulia) wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo baada ya hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio.
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo baada ya hafla ya Gold Fm kukabidhiwa Leseni ya Utangazaji Vipindi vya Redio.