KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao kwa kumsajili kiungo mkabaji wa kimataifa wa Zambia, Paul Katema, kutoka Red Arrows ya kwao.
Katema mmoja wa viungo bora nchini Zambia, amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Azam FC kuongeza nguvu kwenye eneo hilo kuelekea msimu ujao.
Huyo anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa Azam kuelekea msimu ujao na Mzambia wa tatu baada ya Charles Zulu na Rodgers Kola.
Wengine ni Mkenya Kenneth Muguna na mzawa Edward Manyama.