…………………………………………………………………
– RC Makalla aelekeza Suma JKT kuanza Ujenzi Mara moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Cha Shilingi Milioni 100 kwaajili ya Ujenzi wa Paa la Kisasa la kuzuia Jua na Mvua kwa Wahanga 1,800 wa Soko la Kariakoo waliohamishiwa Machinga Complex ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amethibitisha kupokea fedha hizo.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao, RC Makalla amesema baada ya Jana kuwatembelea na kuwasikiliza, Rais Samia aliona changamoto hiyo na alipomuuliza RC Makalla kiasi Cha fedha kinachohitajika alisema ni Milioni 62 za Ujenzi wa Paa la Turubai lakini kwa kutambua umuhimu wa Wafanyabiashara Rais Samia alitoa Milioni 100 ili lijengwe Paa la Kudumu kwa Bati la Kisasa.
Kutoka na fedha kupatikana, RC Makalla amewaelekeza Suma JKT ambao ndio wajenzi kuanza Ujenzi Mara moja ili Wafanyabiashara hao wafanye biashara bila kero.
Kuhusu suala la Meza, RC Makalla amesema tayari amepatikana Mkandarasi atakaejenga Meza za kisasa za kuhamishika kuendana na hadhi ya Soko.
Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Jiji la Ilala kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Taka, Mifumo ya Maji, Mifumo ya umeme na wafunge Vizima Moto ili kukabiliana na majanga ya Moto.