Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Boniface Kadili (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kushoto) wakati Naibu Waziri alipotembelea Programu hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Boniface Kadili (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul vifaa mbalimbali vilivyotumika katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika wakati Naibu Waziri alipotembelea Programu hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul akisaini kitabu cha wageni wakati Naibu Waziri alipotembelea Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Boniface Kadili (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul wakati Naibu Waziri alipotembelea Programu hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wakimfuatilia kwa makini Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri alipotembelea Programu hiyo kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) akipata maelezo toka kwa Mhandisi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa. (SUMA JKT) wakati Naibu Waziri alipotembelea Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Moja ya jengo liilotumika kama Ofisi za wanaharakati wa ukombozi wa Bara la Afrika ambalo kwa sasa linafanyiwa ukarabati.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam
20 Julai, 2021