MKUU wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas akizindua Huduma za kulaza wagonjwa na upasuaji wa Dharula katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa leo kulia ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw. Christopher Komba.
********************************
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, leo imezindua rasmi na kuanza kutoa, huduma za kulaza wagonjwa na Upasuaji wa Dharula, katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa iliyojengwa katika Kijiji cha Nangombo, Kata ya Kilosa Wilayani Hapa.
Akizindua Huduma hizo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kanali Laban Thomas, amewata watumishi na wahudumu wa Afya Wilayani hapa kutoa huduma bora kwa Wazee, na wananchi na wanaofika kupata huduma za matibabu katika Hospitali ya Wilaya, na kufanya kazi kwa bidii na kufuata maadili ya kazi pamoja na viapo walivyokula.
Kanali laban amefafanua kuwa , mara baada ya kuanza kutoa huduma ya kulaza wagonjwa, na Upasuaji wa Dharula, ni mategemeo yake kuwa, huduma zitaboreshwa, na wananchi watapata huduma bora za afya, na Wazee watathaminiwa zaidi ili kuwaenzi, kwa kazi walizofanya kipindi wakiwa vijana za kulijenga Taifa la Tanzania.
Ameongeza kuwa atafurahi zaidi atakapoona Wazee wakipewa huduma bila kuwabagua, wala kuwasumbua, kwa kuwa nao wamechangia huduma nyingi za kulijenga Taifa letu, na kuwataka watumishi, kutoa Huduma kwa kufuata Sheria Taratibu na Kanuni kwa kuzingatia Viapo walipoapa.
“Ndugu wananchi wa Wilaya ya Nyasa na Watumishi wa Afya, leo tukiwa tunafungua Huduma hizi za Kulaza wagonjwa, ninawataka, kuwapa Huduma bora wazee ambao nimewaalika leo, katika Zoezi hili ili waone tunavyozindua huduma hizi, na ninawaagiza wazee hawa tunatakiwa kuwajali kwa kuwapa huduma bora, kwa kuwa nao walishafanya kazi za kulijenga Taifa .Aidha watumishi na Wahudumu wa Afya mnatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa na wateja kwa kuwa wagonjwa wanahitaji hata faraja kutoka kwa Mtoa Huduma za Afya”. Amesema Kanali Thomas.
Awali akisoma Taarifa ya Uzinduzi wa Huduma za kulaza wagojwa na Upasuaji wa Dharula, katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa, Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Nyasa Bw.Sixbert Maseti Ndunguru amesema, mara baada ya Uzinduzi huo, wamejipanga kuhakikisha kuwa, watatoa Huduma Bora kwa Wananchi wa Wilaya ya Nyasa wapatao 140,000, na wananchi wa wilaya jirani za Nchi ya Msumbiji, kupunguza Vifo vitokanavyo na Uzazi kwa kutoa Huduma Za dharula za upasuaji, kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa kutoa huduma elimu za afya na matibabu bora ya Ugonjwa wa kisukari , shinikizo la Damu, kansa kwa kuanzisha kliniki za kila wiki.
Amezitaja huduma zingine ni Dawa muhimu na Vitenganishi vya maabara kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kununua Dawa,Vifaatiba na Vitendanishi kwa wakati.
Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Nyasa wameipongeza Serikali kwa Kuwatatulia changamoto ya Huduma za kulazwa wagonjwa na Upasuaji wa Dharula kwa kuwa awali Hudumahizi walikuwa wakisafiri Umbali Mrefu wa Kilometa 150 kupata matibabu katika hospitali ya Peramiho na songea.
Halmashauri ya Nyasa imekamilisha majengo saba ya awali ya Utawala, maabara, stoo ya dawa,mionzi,wodi ya wazazi,na jingo la kufulia, njia za kuunganisha majengo,Ujenzi ambao umegharimu Tsh Bilioni 2.291, na ujenzi wa Wodi ya Wanaume wanawake na watoto Unaendelea.Mradi huu wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unatarajiwa kuwa na majengo 22 ambayo yatagharimu Tsh Bilioni 7.5.