Afisa Mahusiano Infinix Bi. Aisha Karupa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
*********************
Kampuni ya simu za mkononi Infinix bado inaendelea kuwapa raha wateja wake kupitia kurasa ya Instagram @infinixmobiletz imewajuza wateja wake kuhusu ile promosheni ya Big Mnyana ambapo awamu hii wateja wa Infinix NOTE 10 na NOTE 10 pro watapata nafasi ya kushuhudia michezo mbalimbali ikiwemo ngoma za asili, kuimba kutoka kwenye vikundi mbalimbali vya Sanaa.
Inaeelezwa kuwa ukinunua Infinix NOTE 10 unazawadiwa zawadi hapo hapo ikiwemo Blenda, Jagi La Umeme, Wireless Earphone na Music System.
Akizungumzia Promosheni hiyo Afisa Mahusiano Infinix Bi. Aisha Karupa, amesema kuwa kama ilivyo awali wateja wa kwanza wa Infinix NOTE 10 na NOTE 10 pro kuzawadiwa papo hapo blenda, jagi la umeme, wireless earphone, na music system.
Amesema kuwa Infinix NOTE 10 Big Mnyama ilianza rasmi 13/7/2021 na itaendelea hadi 26/7/2021 katika maduka yote ya simu yenye promosheni ambayo ni Infinix Smart Hub China Plaza Kariakoo, Infinix Smart Hub Mlimani n.k.
Infinix NOTE 10 ni simu mpya inayotamba sokoni kutokana na uwezo wake wa processor ya MediaTek Helio G95 ambayo inaifanya simu hii kuwa nyepesi na yenye kuendesha application za simu hiyo kwa haraka na wepesi pasipo kupata moto.
Infinix NOTE 10 inaaminika kuwa simu sahihi kwa vijana hasa wanafunzi kutokana na GB 8 ya Ram na GB 128 ya Rom kuwa na nafasi ya kutosha kwajili ya kuhifadhi masomo lakini pia ni simu sahihi kwa mfanyakazi wa ofisini kamera ya Infinix yenye MP 64 nyuma inauwezo wa kuscan documenti.
Usipitwe na ofa hizi tembelea maduka ya Infinix Smart Hub Kariakoo na Infinix Smart Hub Mlimani City kuanzia tarehe 20/7/2021.