Klabu ya KMC FC imevuja kambi yake rasmi leo ikiwa ni baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu soka Tanzania bara 2020/2021 ulioanza Septemba mwaka jana hadi hapo msimu mpya utakapoanza wa 2021/2022.
Katika kipindi cha msimu huu KMC FC imefanikiwa kumaliza ligi katika nafasi ya tano hatua ambayo nimafanikio makubwa kwa klabu ya Manispaa ya Kinondoni licha ya kwamba mpango mkakati ulikuwa kumaliza katika nafasi Nne za juu.
Kufuatia matokeo hayo, uongozi unatoapongezi kwa wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu John Simkoko kwa jitihada kubwa walizozifanya katika kuhakikisha kwamba Timu inafanya vizuri katika msimu huu na hivyo kuendelea kuleta chachu kwa mashabiki pamoja na Watanzaia kwa ujumla.
“Ligi imemalizika salama tunamshukuru mwenyezi Mungu, ukiangalia msimu huu ulikuwa na ushindani mkubwa, lakini vijana wetu wamepambana kuhakikisha Timu inabaki kwenye nafasi nzuri, pongezi nyingi ziende kwa benchi zima la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu John Simkoko.
Katika msimu wa 2020/2021, KMC FC imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tano wa msimamo wa ligi Kuu soka Tanzania Bara ikiwa na alama 48, na kufunga magoli 39 ambapo katika msimu wa 2019/2020 ilimaliza ligi katika nafasi ya 13 ikiwa na alama 46, pamoja na magoli ya kufunga 12.
Imetolewa leo Julai 19
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mahusiano wa KMC FC.