Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri (katikati) akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Viwandani kulipotokea moto usiku wa kuamkia leo tarehe 18 Julai, 2021 na kuteketeza nyumba moja inayomilikiwa na Bw. Abdully Mstahafu na sehemu ya nyumba moja ya kulala wageni inayojulikana kama Holiday Guest House. Kulia ni Mheshimiwa Jafari Mwanyemba, Diwani wa Kata ya Viwandani ulipo mtaa huo, na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (M) Dodoma Deogratias Inano (kushoto).
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Dododma (OC-CID), Mrakibu Msaidizi wa Polisi Phillip Mwesigwa (kushoto) akishauriana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri (kulia), Diwani wa Kata ya Viwandani Mhe. Jafari Mwanyemba na Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji Deogratias Inano katika zoezi la Uchunguzi wa Moto uliotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 18 Julai, 2021 katika Mtaa wa Baruti Kata ya Viwandani, jijini Dodoma.
Baadhi ya magari yaliyokuwa yameegeshwa kwa ajili ya matengenezo pembeni ya nyumba zilizoungua moto usiku wa kuamkia leo tarehe 18 Julai, 2021 katika Mtaa wa Baruti Kata ya Viwandani jijini Dodoma yakiwa yamepata madhara kama inavyoonekana kutokana na moto huo. Sehemu hiyo baadhi ya nyumba za kuishi zimegeuzwa matumizi na kuwa maghala ya kuhifadhia vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na maduka ya spea za magari.
Sehemu ya mbele ya moja ya nyumba iliyoteketea kwa moto iliyokuwa biashara ya spea za magari ikiwa imeathirika na moto huo uliotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 18 Julai, 2021 mtaa wa Baruti kata ya Viwandani Jijini Dodoma.