****************
TIMU ya Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutwaa tena taji la Ligi ya Mbingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini usiku huu Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Iliwabidi Ahly kusubiri hadi beki wa Kaizer Chiefs, Happy Mashiane atolewe kwa kadi nyekundu dakika ya 45 ili kuanza kushangilia mabao yao yaliyowapa taji la 10 la michuano hiyo.