Home Mchanganyiko RAIS MHE.DKT. MWINYI AMJULIA HALI WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA WANANCHI...

RAIS MHE.DKT. MWINYI AMJULIA HALI WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA WANANCHI WALIOLAZWA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA JIJINI ZANZIBAR.

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali mmoja wa Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja  Ndg. Said Mussa, aliyelazwa katika Wodi ya Wagonjwa wa mifupa. (Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.Dr.Msafiri Marijani, alipowasili katika viwanja vya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwatembelea na kuwajulia hali Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali Mtoto Samir Haji akiwa amepakatwa na Mama yake Bi. Zulfa Vuai Mwinyi, alipotembelea Wodi ya Watoto katika jengo la Taasisi ya ‘ Neurosurgical Institute’ katika Hopitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimjulia hali Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar. Mhe. Nassor Ahmed Mazrui aliyelazwa katika  la Wodi ya Taasisi ya ‘Neurosurgical Institute’ katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)