Home Mchanganyiko WATURUKI WAWAKUMBUKA WALIOKUFA MASHAHIDI KATIKA JARIBIO LA MAPINDUZI NCHINI MWAO

WATURUKI WAWAKUMBUKA WALIOKUFA MASHAHIDI KATIKA JARIBIO LA MAPINDUZI NCHINI MWAO

0

*************************

Balozi  wa  Uturuki  hapa  nchini  Mehmet  Gulloglu  ameyaomba Mataifa Mengine Kutilia Mkazo wa Kudhibiti watu wanaoweza Kufanya Majaribio ya Uasi wa Serikali kama Ilivyo Fanyika Nchi  Mwao July 15  Mwaka  2015.

Hayo  ameyaeleza  leo Jijini  Dar es Salaam  katika  kumbukizi ya miaka  sita  ya  taifa  la uturuki  ya   kuwakumbuka  mashahidi waliofanikisha  kuzuia  mapinduzi  yaliyotaka  kumpindua  rais  wa  taifa  hilo Reccep Tayyip Erdogan.

Balozi  Mehmet  amesema usiku huo  utakumbukwa  kutokana  na mashahidi  amabao  ni wananchi  waliweza  kuyazuia  mapinduzi  hayo  bila  kuwa  na  silaha  japo  waliotaka  kufanya  mapinduzi hayo  walimiliki kila  aina ya  silaha ya kivita.

Balozi  huyo  wa Uturuki  hapa  nchini  amesema katika  siku  hiyo watu  mia mbili  na hamsini  walikufa huku  maelfu ya  watu  wakiachwa  majeruhi .

Mbali  na  kuzungumzia  siku  hiyo  Balozi  Mehmet amelilaani  kundi  lililojaribu kufanya  mapiduzi  hayo huku akitoa tahari kwa mataifa  mengine  kuwa  makini  na makundi  kama  hayo  kwani yanaweza kuleta madhara  popote  ulimwenguni.

Kumbukumbu  hiyo  imekwenda  sambamba  na uzinduzi  rasmi  wa kisima cha maji kilichokuwa  katika  bustani  ya  Drive inn  iliyopo  katikati ya  jiji la  Dar es Salaam  Kisima  kilichokuwa  na  kumbukumbu  ya  Profesa  Dakta  Ilhan  Varank  moja  kati  ya  watu walioheshimiwa  nchini Uturuki.