*************************
Balozi wa Uturuki hapa nchini Mehmet Gulloglu ameyaomba Mataifa Mengine Kutilia Mkazo wa Kudhibiti watu wanaoweza Kufanya Majaribio ya Uasi wa Serikali kama Ilivyo Fanyika Nchi Mwao July 15 Mwaka 2015.
Hayo ameyaeleza leo Jijini Dar es Salaam katika kumbukizi ya miaka sita ya taifa la uturuki ya kuwakumbuka mashahidi waliofanikisha kuzuia mapinduzi yaliyotaka kumpindua rais wa taifa hilo Reccep Tayyip Erdogan.
Balozi Mehmet amesema usiku huo utakumbukwa kutokana na mashahidi amabao ni wananchi waliweza kuyazuia mapinduzi hayo bila kuwa na silaha japo waliotaka kufanya mapinduzi hayo walimiliki kila aina ya silaha ya kivita.
Balozi huyo wa Uturuki hapa nchini amesema katika siku hiyo watu mia mbili na hamsini walikufa huku maelfu ya watu wakiachwa majeruhi .
Mbali na kuzungumzia siku hiyo Balozi Mehmet amelilaani kundi lililojaribu kufanya mapiduzi hayo huku akitoa tahari kwa mataifa mengine kuwa makini na makundi kama hayo kwani yanaweza kuleta madhara popote ulimwenguni.
Kumbukumbu hiyo imekwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa kisima cha maji kilichokuwa katika bustani ya Drive inn iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam Kisima kilichokuwa na kumbukumbu ya Profesa Dakta Ilhan Varank moja kati ya watu walioheshimiwa nchini Uturuki.