Kamisha Mkuu wa TRA Alfayo Kadata akizugumza na wafanyabiashara jijini Arusha.picha Happy Lazaro)
Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongela akizungumza na wafanyabiashara jijini Arusha.(Happy Lazaro).
****************************
Happy Lazaro,Arusha
Mamlaka ya mapato Tanzania imetangaza kuanza kutumia sheria katika kutoa adhabu kwa wale wote watakao kaidi kutoa au kudai risiti kwakuwa wamekuwa wakichangia upotevu wa mapato ya serikali hali inayodidimiza uchumi na kukosa maendeleo ya nchi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata ameyasema hayo katika mkutano wa TRA na walipa Kodi Jiijini Arusha wakiwemo wafanyabiashara pamoja na wakuu wa Taasisi mbalimbali .
” Kuanzia Sasa tutatumia Sheria zetu kutoa adhabu Kali kwa wale wasiotoa risiti no vizuri tuwe na utamaduni wa kudai risiti kwani endapo utabainika itachukuliwa hatua kali “amesema
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akizugumza katika mkutano huo , amewataka wakazi wa mkoa wa Arusha kushirikiana katika kufichua biashara ya bidhaa bandia ambazo zimekuwa zikichangia kudidimiza uchumi .
“Bado Mkoa wetu unatumika Kama daraja la bidhaa za kughushi kwa hiyo sisi Kama Mkoa wa Arusha tunatakiwa kushirikiana na Kuendelea kuhamasisha kuepuka kufanya biashara za bidhaa za kughushi “amesema
Naye Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Kelvin Remen amesema mkutano huo ni jukwaa muhimu litakalo wasaidia wafabishara kulipa kodi kwa njia rafiki bila kuwa na matatizo yeyote kwa wafanyabiashara.
“Hii ni fursa kwa walipa Kodi kupata nafasi ya kukaa na uongozi wa juu wa TRA ilinkuwaeleza Changamoto zetu ili kuweza kufikia malengo yetu na Taifa pasipo kumwumiza mfanyabiashara yeyote “alisema
Mkutano huu wa siku mbili Kati ya TRA na walipa Kodi umelenga kuinua uchumi na kuimarisha matumizi sahihi mashine za kielekroniki kwa wafanyabiashara na wateja hasa katika kuinua uchumi wa Nchi .