Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato (wa pili kulia) akizungumza na wanakijiji cha Ilangu wakati wa uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato (wa pili kulia) akizindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato (wa pili kulia) akimtambulisha mkandarasi wa ujenzi wa umeme kwa wanakijiji cha Ilangu wakati wa Uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati, TANESCO na REA mara baada ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi
Wanakijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato (hayumo pichani) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato (aliyekaa katikati) akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Tanganyika (wa kwanza kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili iliyofanyika katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi
………………………………………………………………………………..
- Zaidi ya shilingi bilioni 15 kutumika kuvipelekea umeme vijiji 25 katika wilaya ya Tanganyika.
Na Dorina G. Makaya – Katavi
Naibu Waziri wa Nishati tarehe 13 Julai, 2021, amefanya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya III Mzunguko wa pili katika kijiji cha Ilangu, kata ya Ilangu, tarafa ya Kabungu, wilaya ya Tanganyika, mkoa wa Katavi.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Naibu Waziri Byabato amesema, zaidi ya shilingi bilioni 15 zitatumika kuvipelekea umeme vijiji 25 vya wilaya ya Tanganyika.
Amesema, kwa kijiji cha Ilangu peke yake, takriban shilingi millioni 618 zitatumika kuunganisha umeme.
Amesema, serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji umeme nchi nzima na kuwa upatikanaji wa umeme vijijini utachangia kuongezeka kwa kasi ya uanzishwaji wa viwanda vya uchakataji wa mazao na kuwa kichocheo cha ukuaji wa biashara na uchumi kiujumla.
Naibu Waziri Byabato amewaambia wanakijiji cha Ilangu kuwa, Serikali imewapunguzia wananchi gharama ya kuunganishiwa umeme kutoka shilingi 177,000 hadi shilingi 27,000 tu kwa wateja wa umeme wa njia moja na kwa wateja wa umeme wa njia tatu kutoka shilingi 912,000 hadi shilingi 139,500 ili kuwawezesha wananchi kuunganishiwa umeme.
Amesema, kwa mwananchi ambaye atakuwa hajakamilisha kupata pesa kamili za kulipia anaweza kulipa kidogo kidogo ndani ya kipindi cha Mradi wa eneo husika na atakapokamilisha ataunganishiwa umeme.
Naibu Waziri Byabato amemtaka mkandarasi wa Mradi kuhakikisha anawaunganishia umeme wateja wote bila kujali aina ya nyumba anayoishi na kutoa kipaumbele kwa taasisi na maeneo yanayotoa huduma za kijamii kama vile vituo vya afya, shule, nyumba za ibada, ofisi za Serikali, visima vya maji pamoja na viwanda vidogo ambavyo vitachangia kasi ya maendeleo katika eneo husika na Taifa kiujumla.
Ameeleza kuwa, kupatikana kwa umeme katika kata ya Ilangu pamoja na maeneo mengine ya vijiji ambavyo bado havijaunganishiwa umeme, kutachochea ukuaji wa viwanda vikiwemo vya kuchakata mazao, vya kusaga na vya uchomeleaji.
Naibu Waziri Byabato amesema, ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda kulipia gharama za kuunganishiwa umeme, Serikali imemuelekeza Mkandarasi kufungua ofisi katika eneo linalotekelezwa mradi na kuwa hakuna mwananchi anayetakiwa kulipia nguzo.
Amewaasa wananchi kutunza miundo mbinu ya umeme na kubainisha kuwa, Mradi wa REA hauna fidia.
Amewaomba wananchi wa eneo la mradi kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi na kuwataka kutumia fursa hiyo kujipatia ajira za muda.
Amewaasa wanakijiji hao, kuepuka tabia ya kuharibu miundo mbinu ya umeme ili kuhakikisha umeme unaendelea kupatikana.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Rojers Romuli, ameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuvipelekea umeme vijiji vya Halmashauri ya Tanganyika na kusema kuwa, hatua hiyo itachangia katika kuongezeka kwa kasi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Naye mbunge wa jimbo la Tanganyika Mkoa wa Katavi Mhe. Moshi Kakoso amewataka wanakijiji cha Ilangu na wananchi wote wa jimbo la Tanganyika kuitumia vema fursa ya kuja kwa umeme jimboni humo ili kujiletea maendeleo.
Jumla ya shilingi bilioni 24.7 zitatumika kuviunganishia umeme vijiji 53 ambavyo bado vilikuwa havijapata umeme katika mkoa wa Katavi