Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simyu wakiwa katia mkutano na waandishi wa Habari.
Kuanzia kulia Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo, Mkuu wa Mkoa Mhe. David Kafulila na Meneja Mradi Ujenzi wa reli ya kisasa Mwanza- Isaka Eng. Machibya Masanja wakiwa katika kikao na waandishi wa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo wakati wa kikao na Waandishi wa habari.
******************************
NA SARAH KIBONDE, SIMIYU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.David Kafulila amempongeza Rais kwa kuendeleza ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha Mwanza hadi Isaka kwa kasi zaidi ambapo gharama zinakazokamilisha mradi huo ni shilingi Trilioni 3.
Hayo ameleza jana wakati akifungua kampeni ya kuhamasisha uelewa wa wananchi kuhusu mradi wa SGR kipande cha Mwanza – Isaka( 341km), ambapo amesema gharama hiyo ni nafuu kulinganisha na Kenya na hata Ethiopia na hivyo inathibitisha usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali.
“Hii inazidi kuthibitisha ripoti ya jukwaa la kimataifa kuhusu uchumi- World Economic Forum 2019 kuonesha kwamba Tanzania ni nchi ya 29 katika nchi 186 duniani katika usimamizi thabiti wa matumizi ya fedha za umma”. Alisema RC Kafulila.
Aidha amewahakikishia wananchi kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria na zaidi kuwaomba wachangamkie fursa za biashara wakati wa ujenzi hususan eneo la Malampaka ambapo kambi kubwa ya ujenzi zinajengwa.
Alisisitiza Shirika la reli kutoa upendeleo kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu kwa kazi ambazo zipo ndani ya uwezo.