TANZANIA imepangwa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, CECAFA Challenge U23 inayotarajiwa kufanyika Ethiopia baadaye mwezi huu.
Tanzania imepangwa pamoja na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wenyeji, Ethiopia wapo Kundi B pamoja na Burundi na Eritrea.
Kundi C linazikutanisha U23 za Kenya, Sudan Kusini na Djibouti katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Julai 18 hadi 30, mwaka huu.
Vinara wa makundi yote wataingia Nusu Fainali pamoja na timu itakayomaliza na wastani mzuri zaidi katika nafasi ya pili.
MAKUNDI;
Kundi A: Uganda, Tanzania, DRC
Kundi B: Ethiopia, Burundi, Eritrea
Kundi C: Djibouti, Sudan Kusini, Kenya
RATIBA
Julai 18: Uganda vs DRC
Ethiopia vs Eritrea Julai 19; Djibouti vs Kenya Julai 21; Burundi vs Eritrea
Julai 22; Sudan Kusini vs Kenya
Tanzania vs DRC
Julai 24; Ethiopia vs Burundi
Julai 25; Djibouti vs Sudan Kusiji
Uganda vs Tanzania
NUSU FAINALI
Julai 28; Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Pili Bora
Mshindi Kundi B vs Mshindi Kundi C
FAINALI – Julai 30
MSHINDI WA TATU – Julai 30