Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakisubiri kukabidhiwa leo Mwenge wa uhuru kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo Louis Bura (wa pili kutoka kushoto) akipokea Mwenge wa uhuru leo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalua Paul Chacha(wa pili kutoka kulia) , tayari kwa mbio,
Mkuu wa wilaya ya Urambo Louis Bura akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru leo baada ya kuupokea kutoka Kaliua.
Viongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru wakipitia taarifa mbalimbali kabla ya kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa uzio katika Mnada wa Urambo leo.
Kiongozi wa Mbio hizo Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi akiweka Jiwe la Msingi leo uzinduzi wa ujenzi wa uzio wa Mnada wa Urambo.
Kiongozi wa Mbio hizo Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi akiangalia leo jinsi Wanafunzi wa Shule ya kutwa ya Urambo wanavyotumia TEHAMA kujisomea.
Kiongozi wa Mbio hizo Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi na wenzake wakiangali chanzo cha Maji cha wakazi wa Urambo mjini leo wakati wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio hizo Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi akipanda mti leo katika chanzo cha maji ya mji wa Urambo.
Picha na Tiganya Vincent
……………………………………………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
MIRADI sita yenye thamani ya milioni 967.2 Wilayani Urambo imezinduliwa na mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru.
Kati ya miaradi hiyo Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi milioni 831.3 na, Halmashauri imechangia 134.9.
Kiongozi wa Mbio hizo Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi amezindua miradi hiyo baada ya kuikagua katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Urambo.
Mradi wa kwanza aliweka jiwe la Msingi ni wa ujenzi wa uzio wa wa Mnada wa Mifugo Urambo ambao umegharimu shilingi milioni 134.7.
Amesema baada kujengwa kwa uzio huo na kufanikiwa kuongeza makusanyo ya siku kutoka wastani wa laki 6 hadi kufikia milioni 1.4 ni vema wakatumia fedha hizo kuboresha zaidi mazingira ya Manada huo.
Luteni Mwambashi amezindua pia mradi wa Ujenzi wa barabara ya lami 0.81km katika Mji wa Urambo yenye thamani milioni 416.
Akikagua chumba cha mradi wa TEHAMA katika shule ya sekondari Urambo uliogharimu milioni 10,amewataka wananfunzi wa Shule hiyo kutumia fursa hiyo kujiendeleza Kitaalum.
Luteni Mwambashi ameweka jiwe la msingi Ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Itebulanda wenye gharama yenye milioni 230 kwa kuwataka Wasimamizi wa Mradi huo kuhakikisha wanaujenga kwa viwango vinavyotakiwa na kuukamilisha kwa wakati ili usaidie kupunguza adha kwa wananchi kufuata maji yasiyo salama umbali mrefu.
Aidha Mwenge wa uhuru ulikagua matumizi ya mfumo wa kielekitroniki wa usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya (Got HOMIS) ambao umefungwa kwa gharama ya shilingi milioni 25.3 na kujionea jinsi ulivyoongeza makusanyo ya Serikali kutoka Laki tano kwa Mwezi na kufikia wastani milioni 4
Kiongozi huyo wa Mbio hizo Maalumu za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine amewaagiza wasiamimizi wa miradi kuhakikisha kunakuwepo na taarifa zote muhimu ili kuepuka usumbufu.