Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba akizungumza Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw.Sabasaba Moshingi akizungumza Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt Edmund Mndolwa akizungumza Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja akizungumza Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba akizindua Benki mpya ya TCB ambao hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt Edmund Mndolwa akimpatia zawadi maalumu Waziri wa Fedha na Mipango Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw.Sabasaba Moshingi akimkabidhi mfano wa kadi mpya ya Benki ya TCB Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TPB Bw.Sabasaba Moshingi akimpatia kadi mpya ya Benki ya TCB Waziri wa Fedha na mipango Dkt.Mwigulu Nchemba Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba akionesha kadi mpya ya Benki ya TCB mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TPB Bw.Sabasaba Moshingi Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba akipata picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya TCB Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba amewataka watumishi wa Benki mpya ya TCB kuhakikisha wanalitendea haki jina la Benki hiyo huku akisema uwezo wa kuipaisha Benki hiyo ipo mikononi mwao zaidi wanapaswa kuongeza ubunifu na kujiandaa kiushindani.
Ameyasema hayo leo Katika hafla ya uzinduzi wa Benki mpya ya TCB (Tanzania Commerce Bank) iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema moja ya changamoto nyingi zinazoipata taasisi za kiushindani ni kuziba mianya ya ubunifu na kutegemea mbelekeo ya Serikali na hivyo kujikuta zikianguka.
“Sekta ya kibenkinkwa Tanzania bado haijaweza kugikia ngazi ya kikanda na kimataifavhatua inayotokana na benki zenyewe kushindwa kujitangaza katika nchi hizo hususan mataifa ambayo yanafanya biashara au usafirishaji na Tanzania”. Amesema Waziri Nchemba.
Aidha ameyataka mabenki kutoka nchini na kwenda kuwekeza katika nchi zingine ili kuongeza ushindani wa kibiashara na hivyo kujiongezea faida.
“Serikali inakwenda kuchochea ukwasi kwenye uchumi hatua ambayo itazisaidia Benki kupata idadi kubwa ya wateja”. Amesema Waziri Nchemba.
Nae mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Dkt.Edmund Mndolwa ameishukuru serikali kwa juhudi inazozifanya katika kuimarisha sekta ya kifedha ikiongeza matumizi ya mifumo ya kifedha ambayo imesaidia Serikali kuongeza mapato.
“Kuongezeka kwa mapato hayo kumeiwezesha Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yq kimaendeleo kutokana na fedha zinazopatikana kutokana na ujio wa mifumo hiyo”. Amesema Dkt.Mndolwa.
Amesema TPB kupitia maboresho ya huduma zake mbalimbali umesaidia kupiga hatua za kimaendeleo ambapo tangu iunganishwe na Benki mbalimbali ikiwemo TIB na Benki ya Wanawake kimeiwezesha Benki hiyo kuongeza ufanisi wake.