Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama akiwa anacheza mpira katika mazoezi yaliyowahusisha watumishi wa Tume hiyo, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama akiwa na watumishi wengine wa Tume hiyo wakati wa mazoezi.
Baadhi ya Watumishi wa TSC wakiwa wanafanya mazoezi katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma, jijini Dodoma.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa TSC waliohudhuria mazoezi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Paulina Nkwama akiwa na watumishi wengine wa Tume hiyo wakati wa mazoezi.
**********************************
Katika jitihada za kuimarisha afya na kuongeza ufanisi zaidi wa utendaji kazi kwa watumishi wake, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishiwa Walimu (PO-TSC), imejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku ya Ijumaa kuanzia saa kumi na nusu jioni.
Akiongoza mazoezi hayo kwa watumishi, Katibu wa PO-TSC, Paulina Nkwama alieleza kuwa ofisi yake imekuwa ikiunga mkono agizo la Serikali la kufanya mazoezi ikiwa ni moja ya njia za kujikinga na magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza na kuimarisha afya.
Aliongeza kuwa pamoja na kuimarisha afya, watumishi hao wanapokutana na kufanya mazoezi kwa pamoja inawasaidia kujenga upendo na ushirikiano miongoni mwao na hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
“Naendelea kuwasisitiza tujitokeze kwa wingi kwenye mazoezi na michezo kwani michezo na mazoezi ni afya, ni urafiki, ni ajira kwa wasio na ajira, na pia ni mshikamano.” Alisema Nkwama
Mazoezi hayo yanayofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma