Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge (katikati) akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya mbio za Mwenge wa Uhuru wakati wa akikagua Miradi ya Mwenge wa Uhuru itakayozinduliwa, kufunguliwa ,kuwekewe mawe ya msingi na kutembelewa.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amekagua Miradi ya Mwenge wa Uhuru itakayozinduliwa, kufunguliwa ,kuwekewe mawe ya msingi na kutembelewa.
Akikagua eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkoa wa Singida na Tabora i
Malendi Wilaya ya Iramba Mahenge amewaomba wananchi, viongozi wa dini, Siasa, mashirika naTaasisi za Serikali na binafsi,vyama vya wafanyakazi pamoja na watumishi kushiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika Tarehe 20/07/2021 na maeneo yote ya miradi pamoja mikesha.
Mkuu wa Mkoa amewahakikishia Wananchi kuwa tahadhari zote za ugonjwa wa corona zitachukuliwa muda wote hadi Mwenge wa Uhuru utakapo kabidhiwa Mkoa wa Dodoma Tarehe 25/07/2021.
Mratibu Mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani ambaye ni Afisa Vijana mkoa amemuhakishia mkuu wa mkoa wa Singida kuwa maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika katika wilaya zote za mkoa kwa ujumla.
Mwenge huo katika Mkoa wa Singida utakimbizwa katika wilaya tano za kiutawala ambazo ni Iramba, Mkalama, Singida, Ikungi na Manyoni.