RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na (kulia kwake) Mkurugenzi Mkuu wa Sauti za Busara Zanzibar Bw.Yussuf Mahmoudu, walipofika kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Sauti za Busara Zanzibar ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mhe. Simai Mohammed Said (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na wageni wake Ujumbe wa Uongozi wa Sauti za Busara Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhe. Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)