Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), CPA (T) Evance Assenga,akitoa neno la shukrani kwa Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,mara baada ya kufungua mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,(hayupo pichani) wakati akifungua akifafanua mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Ernest Mwaswaliba kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,akitoa mada wakati wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akiwa katika picha za pamoja na washiriki mara baada ya kufungua mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
MENEJIMENTI ya Tume ya maendeleo imetakiwa kuzingatia mifumo ya udhibiti iliyowekwa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha sheria,kanuni, taratibu na miongozo inazingatiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Hayo yamesemwa leo Julai 13,2021 na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC) Dkt. Benson Ndiege wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika jijini Dodoma.
Dkt.Ndiege amesema Menejimenti hiyo inatakiwa kuzingatia mifumo ya udhibiti iliyowekwa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha sheria, kanuni, taratibu na miongozo inazingatiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
“Ni jukumu la Menejimenti kuhakikisha kuwa kazi zinatekelezwa kwa kuzingatia malengo ya Tume, mipango na mikakati ya utekelezaji wa majukumu inazingatiwa na inatekelezwa ipasavyo na kunakuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za Tume,”amesema Dkt.Ndiege
Mrajisi huyo amesema Kamati ya Ukaguzi ni chombo muhimu chenye jukumu la kusimamia kazi za ukaguzi wa ndani kiufundi na kumshauri Afisa Masuuli kuhusu Udhibiti wa Ndani , Menejimenti ya Vihatarishi na Utawala Bora ili kuiwezesha Tume kufikia malengo yake.
“Ili Kamati iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ni muhimu Kamati ifanye kazi kwa weleledi na ufanisi. Hivyo, mafunzo haya ninayoyazindua leo yanatarajiwa kuisaidia Kamati kuongeza weledi na ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yake,”amesema
Vilevile,amesema mafunzo haya yataiwezesha Menejimenti ya Tume kuelewa majukumu ya Kamati ya Ukaguzi na pia kujifunza wajibu wa menejimenti kuhusu utekelezaji wa ushauri na mapendekezo yanayotolewa na ya Kamati ya Ukaguzi.
Dkt.Ndiege,amesema ili kazi ya Kamati ya Ukaguzi ya kushauri iwe nyepesi, ni jukumu la Menejimenti ya Tume kuhakikisaha kuwa inaweka mifumo toshelevu na imara ya udhibiti wa ndani ili kuzuia vihatarishi vinavyoweza kusababisha Tume isifikie malengo yake.
Mrajis huyo amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kwa dhati kuendeleza na kuimarisha vyama vya ushirika nchini ili kuleta tija kwa wanachama na hatimaye kuijenga Tanzania yenye uchumi wa kati na wa viwanda kupitia vyama vya ushirika.
“Nina imani kuwa ushirika ukiendeshwa na kusimamiwa vizuri unayo fursa kubwa ya kushiriki katika kujenga, kuimarisha na kustawisha uchumi wa nchi yetu na maisha ya wananchi kwa ujumla,”amesema Dkt.Ndiege
Mrajis huyo amewaomba wajumbe wa Kamati na Menejimenti ya Tume kutumia fursa hiyo vizuri kujifunza ,kuuliza maswali ili kuapata ufafanuzi na kujadiliana kuhusu mada husika ili mafunzo hayo yaweze kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye,Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), CPA (T) Evance Assenga,amesema wanachofanya katika kamati hiyo ni kupitia taarifa za mkaguzi wa ndani na taarifa ua mkaguzi wa nje pamoja na kushauri katika eneo la utawala bora.
“Kwa mujibu wa sheria ya fedha namba 30 inataka Taasisi kuwa na kamati ya ukaguzi,Nipende kukudhibitishia kwamba ofisi yako tayari ina kamati ya ukaguzi na inaenda mwaka wa tatu na inafanya vizuri.
“Kwa mujibu wa sheria inatutaka tukutane mara nne kwa mwaka na haya yote tumeweza kuyatimiza mara zote nne kwa mwaka,”amesema