Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani alipowasili ofisini kwake, Jijini Rabat Julai 13, 2021.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa wa Morocco Nasser Bourita, Katika Mazungumzo hayo aliambatana na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa Jijini Rabat Julai 13, 2021.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa wa Morocco Nasser Bourita, Jijini Rabat Julai 13,2021
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani, baada ya kufanya mazungumzo Jijini Rabat Julai 13, 2021.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani, Jijini Rabat Julai 13, 2021.
****************************
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 12, 2021 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa wa Morocco Nasser Bourita na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani.
Katika Mzungumzo hayo Waziri Mkuu alizungumzia kuimarisha ushirikiano mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na Morocco ulioasisiwa na kujengwa na wasasisi wa nchi hizi mbili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mfalme Mohammed V.
Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa nchi hizi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Kilimo, Utalii, Nishati na Uvuvi.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Leila Muhamed Mussa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.