WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo,akitoa maelekezo kwa Mtaalamu wa Mazingira kutoka kampuni ya Yapi Merkez,Bw.Aminiel Mlugarana mara baada ya kufanya ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo,akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
Meneja Ufundi,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA) Mhandisi Kashilimu Mayunga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo, kufanya ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
Kaimu Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati,Emmanuel Mwasilu,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
Mtaalamu wa Mazingira kutoka kampuni ya Yapi Merkez,Aminiel Mlugarana,akizungumza na waandishi mara baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo, baada ya kufanya ziara ya kukagua Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
Muonekano wa Mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) yaliyopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma leo Julai 12,2021.
…………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo ameonesha kutokuridhishwa na mradi wa mabwawa ya kutibu maji taka katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma ambapo amemtaka Mkandarasi kufuata matakwa ya kimazingira ili kuwalinda wananchi.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 12,2021,wakati wa ziara yake ya kukagua mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Standard Gauge (SGR) uliopo eneo la Zuzu Jijini Dodoma.
Akiwa katika mradi huo Waziri Jafo ameoneshwa kutokuridhishwa na mradi huo huku akihoji ni kwanini hawakufuata masharti ya kimazingira kutoka Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (DUWASA) na Jiji la Dodoma.
Hivyo ametoa maelekezo kwa Mkandarasi kufuata matakwa ya masharti ya kimazingira ili kuwalinda wananchi
“Nitoe maelekezo kwa wakandarasi wengine wenye miradi ya kuchimba mabwawa nchini lazima wafuatilie matakwa ya masharti ya kimazingira kwa sababu lazima tuweke miradi na lazima tuwalinde wananchi ambao tunawawekea miradi hii kiufupi hapa sikuridhika na hichi nilichokiona,”amesema Jafo
Vilevile, ameitaka kampuni hiyo kufuata maelekezo ya Duwasa na watalamu wengine pindi wanapotekeleza miradi mbalinbali katika Jiji la Dodoma.
“Kikubwa sasa mfuate maelekezo mkitoka hapa mtaongea na watu wa Duwasa na watalamu nini mfanye tena nguvu mliyotumia kuchimba haya mashimo mngekuwa sasa hivi mmeishafika mbali,”amesema.
Katika hatua nyingne,Waziri Jafo ameipa wiki mbili kampuni ya Yapi Merkez iwe imefukia mashimo iliyoyachimba kwa ajili ya kutengeneza mabwawa katika eneo la Zuzu kutokana na kutowashirikisha Duwasa na NEMC.
“Hamkwenda Duwasa mmeamua kufanya kazi wenyewe shughuli zenu lazima mfuate masharti ya Serikali lazima mwende NEMC kwahiyo vyote hamkufanya.Nini mpango wenu sasa ?Mtu wa mazingira nataka nijiridhishe lini nitakuja hapa niangalie nawapa wiki mbili nitakuja hapa.
“Huu mradi ni wa kwetu wote lakini vilevile yale masharti lazima tuyafuate tusifanye huu mradi ukaleta adhari kwa watu haiwezekani hapa kuna wakazi wa aina mbalimbali ukiangalia uchafu wa hapa huwezijua inawezekana watoto wa hapa wadogo wanatoroka kuja kufanya kitu tofauti.
“Huwezi jua Duwasa mna jukumu la kusimamia majitaka Ofisi yangu itataka ipate taarifa jinsi gani hizi temrary report zinafanywa na watu wangu wa NEMC fuatilini hili jambo kuhakikisha kila jambo linaenda vizuri,”amesema.
Pia amewataka kujenga miradi ambayo itabaki na wananchi wataitumia hata baada ya kukamilka kwa miradi yao.
“Tujifunze kwanini katika kambi za wakimbizi kunajengwa shule kunajengwa vitu vingine hata wakimbizi wakiondoka mioundombinu inaendelea kutumika tujifuze kwanini Tanrod wakitengeneza barabara kwanini zile nyumba zinazobakia zinatumika katika mindombinu.
“Kuna uharamu gani nyinyi mkapata mtaalamu mkatengeneza mabwawa mkimaliza hapo inakuwa sehemu ya miundombinu Serikali na watu itaendelea kuitumia siku zingine,”amesema
Kwa upande wake,Kaimu Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati,Emmanuel Mwasilu amesema kabla ya Waziri Jafo kufika walifika katika mradi huo na kuonesha kutokuridhishwa na mazingira jinsi yalivyo.
Amesema kutokana na hali hiyo wamewachukua hatua ya kuipiga faini kampuni hiyo ya shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza miundombinu iondoshwe mahali hapo na shughuli isitishwe.
“Wameishasitisha, lakini pia wafanye uchapushaji kuwe katika hali nzuri maelekezo mengine ya Waziri tunayachua kwa ajili ya kuwaelekeza wakandarasi wengine.Nitoe wito kwa wananchi Taasisi mbalimbali na Wakandarasi waweze kufuata sheria na maelekezo ambayo tunakuwa tumewapa katika vibali,”amesema.
Naye,Mtaalamu wa Mazingira kutoka kampuni ya Yapi Merkez,Aminiel Mlugarana amesema watayafunga mabwawa hayo na watashirikiana na Duwasa na NEMC kutafuta eneo jingine kwa ajili ya kufanya shughuli kama hiyo.
“Kama Waziri alivyosema ndani ya wiki mbili tutafanya kitu pamoja na kuyafukia mabwawa haya na kuirudisha ardhi kama ilivyokuwa awali na tutashirikina na Duwasa na NEMC kutafuta eneo kwa ajili ya kufanya shughuli kama hiyo,”amesema.
Kwa upande wake Meneja Ufundi,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA) Mhandisi Kashilimu Mayunga amesema maelekezo ambayo ameyatoa Waziri watayafuata na watashirikiana kuwapa utaalamu wa namna gani ya kuweza kujenga mabwawa hata kama ni ya muda mfupi.