******************
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiambatana na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya CCM Taifa leo tarehe 11 Julai, 2021 ameanza ziara katika mkoa wa Mbeya akitokea Songwe.
Akiwa katika kikao cha mapokezi jijini Mbeya Katibu Mkuu amesisitiza wanaCCM kuhudhuria vikao vya mashina ikiwa ndio msingi wa uimara wa Chama, na kila mwanachama anawajibika katika shina lake.
“Tumekuja huku chini kwenye Mashina kwa sababu huku ndipo kwenye uhai wa Chama Chetu, hapa kwenye Shina tunazungumza na wanachama wote na ndipo penye wananchi.” Katibu Mkuu Chongolo ameeleza
Aidha ameongeza kuwa, “Ukweli ni kwamba sisi wote hapa ni wanachama wa Mashina, hapa hakuna mwanachama wa tawi, kata, wilaya, mkoa wala Makao Makuu, Mwenyekiti wa Chama Chetu ni mwanachama wa Shina, mimi (Katibu Mkuu) ni mwanachama wa Shina, kila mmoja wetu hapa ni mwanachama wa Shina.”
Akiendelea na ziara katika wilaya ya Kyela, Katibu Mkuu ametembelea Shina namba 01 Tawi la Lema, shina namba 02 Tawi la Njisi , shina namba 02 tawi la Nazaleth ambapo ameeleza kwa undani umuhimu wa mikutano ya mashina.
“Tumekuja kuhimiza vikao hivi vya Mashina, kwetu sisi vikao hivi ni muhimu kuliko vikao vyote, kwa kiongozi yeyote mwakani anayetaka kugombea uongozi ndani ya Chama lazima awe na muhtasari wa mahudhurio ya vikao vya mashina.”
Ameongeza kuwa, “Ukiwa mwanachama wa shina, ukaheshimu uongozi wa shina, ukamuheshimu balozi, tukajenga msingi wa kufuata kalenda ya Chama chetu ya vikao, na tukashiriki kwa adabu huku tukimuheshimu Mwenyekiti wa Shina Chama chetu hiki hakitayumba milele.”
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ametemmbelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya upili (High School) ya Lema a Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Huduma ya pamoja Mpakani katika eneo la Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi.
#KaziIendelee.