Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel J. Shilatu (aliyeshika chepe mkononi) akishirikiana na Wananchi kuchanganya zege wa kuweka kwenye msingi ujenzi nyumba ya Daktari Zahanati ya Miuta
……………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu, Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewapongeza na kuwashukuru Wananchi kata ya Miuta na maeneo yote ya Tarafa ya Mihambwe kwa kujitolea kwao kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa leo Julai 11, 2021 wakati alipotembelea kata ya Miuta na kukuta Wananchi wakijitolea kuchimba msingi na kumwaga zege la msingi ujenzi nyumba ya daktari ambapo Gavana Shilatu alijumuika nao kuwaunga mkono.
“Serikali tunapata faraja sana tunapoona Wananchi mnaungana nasi katika kulijenga Taifa letu. Mimi ni shuhuda mnavyojitoa usiku na mchana kuhakikisha miradi inakamilika. Pongezi kwenu Wananchi na viongozi wote wa hapa Miuta na maeneo yote ndani ya Tarafa ya Mihambwe ambapo nyakati zote mmeonyesha ushirikiano kuijenga Tarafa yetu. Kwa kasi hii niliyoiona hapa natumai nyumba hii ya daktari itakamilika mapema sana, hongereni sana.” Alisema Gavana Shilatu.
Gavana Shilatu amehaidi Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuendelea kushirikiana na Wananchi wote kuhakikisha malengo ya ukamilifu wa miradi inayolinga na thamani ya fedha yanatimia.