Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,akizungumza wakati akifungua kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,akipokea risala kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSTA) Emanuel Mwangoka wakati wa kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha walimu wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSTA) Teddy Gilosa,akizungumza wakati wa kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSTA) Emanuel Mwangoka,akisoma risala wakati wa kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,(hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,akiwakabidhi vyeti wanafunzi walimu mwaka wa tatu mara baada ya kufungua kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Deus Seif,amewataka wahitimu wa Ndaki ya Ualimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ili serikali iendelee kuipa imani sekta hiyo katika suala la usimamiaji mitihani ya taifa.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Bw.Seif amesema kuwa umefika wakati sasa wa nyie walimu wa Karne ya 21 kuwa
watii katika katika kazi ya ualimu ili muifanye Kada ya ualimu kuwa bora na kuvutia machoni mwa jamii.
“Msiende kuwa watu wa kuhangaika mtaani,jitumeni kitumieni chama cha
walimu CWT ili muweze kusonga mbele,”amesema Seif.
Hata hivyo Seif amewataka kuitumia Benki ya Mwalimu ili kujiwekea
akiba yao ya baadae kama walimu wa Karne ya 21.
”Ifike wakati Walimu mchangamkie fursa zinazotolewa kwa ajili ya walimu ambazo zitachangia kujiongeza kipato katika kada ya ualimu.
Awali akisoma risala Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSTA) Emanuel Mwangoka amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017 chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vyanzo vya mapato na hivyo kufanya chama kujiendesha kwa michango ya wadau kikiwemo CWT.
Pia, amesema wao kama walimu tarajali wameomba wapewe elimu kuhusiana na Bodi ya walimu Tanzania ili waweze kuifahamu utendaji kazi wao na walimu watanufaikaje na Bodi hiyo.
”kutokana na kujipambanua kurudisha chama hicho mikononi mwa wanachama wenyewe hasa kuendesha shughuli zake kwa ada za wanachama na huku huduma nyingine wakiwategemea walezi wao, hali hiyo imekuwa ngumu kuwa na fedha ya kutosha kutoka huduma zote na kujaziliza vifaa vya steshenari”amesema Mwangoka