WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakikagua ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma kabla hajaweka jiwe la msingi leo Julai 9,2021.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akimsikiliza Msimamizi Mkuu wa Kazi Bw.Msuya Abdulkarim wakati akikagua mradi wa ujenzi wa kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo Julai 9,2021.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote,(UCSAF) Justina Mashiba wakati akitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote inayojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo Julai 9,2021.
Ujenzi wa Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ukiendelea katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akipata maelezo ya Mchoro wa ramani kuhusiana na ujenzi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa Kazi Bw.Msuya Abdulkarim kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote linalojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo Julai 9,2021.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula ,akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akitoa salamu za mkoa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote,(UCSAF) Justina Mashiba,akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Francis Mihayo akielezea Mradi wa ujenzi wa Ofisi za UCSAF hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji Watumishi housing Dkt.Fred Msemwa,akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Prof.Godliving Mtui,akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akikata utepe kuashiria uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akizundua ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ,(UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 9,2021 katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma.
……………………………………………………..
Na Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dkt Faustine Ndugulile amezindua jengo la Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo ameridhishwa na gharama ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.
Akizungumza leo Julai 9,2021,wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mfuko huo katika eneo la Ndejengwa Jijini Dodoma,Waziri Ndugulile ameridhishwa na shilingi bilioni 2 zitakazotumika katika ujenzi huo.
“Kwa gharama hii niseme nimeridhika naamini tutapata ‘value for Money’ kikubwa nisisitize Desemba tunaleta mgeni rasmi kuja kuzindua, kazi imeisha au haijaisha tunakuja kuzindua jengo lilokamilika inyeshe mvua liwake jua,litoke tetemeko ama ije athari yoyote Desemba tunazindua na sisi tunaanza kufanya mwaliko wa kuwapanga wageni rasmi shughuli hii lazima ifanywe na watu wenye hadhi hiyo,”amesema.
Dkt.Ndugulile amesema Dodoma kwa sasa ndio Makao Makuu hivyo wanahitaji kuweka miundombinu ya kudumu hivyo amewapongeza UCSAF kwa kujenga jengo hilo Mkoani humo.
“Kama alivyotoka kuongea mkuu wa Mkoa kwa sasa Dodoma ni Makao Mkuu tunahitaji kuweka miundombinu ya kudumu niwapongeze sana Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kwa udhubutu na kuanza kazi hii ya kuweka makao makuu ya kudumu hongereni sana,”amesema.
Hata hivyo amesema Mfuko wa Mawasilino kwa wote ulianzishwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2007 lakini walianza majukumu na operation zake mwaka 2009
Amesema Majukumu yake ni kuhakikisha wanapeleka mawasiliano maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara na maeneo ya pembezoni mwa nchi ambapo amedai kuna Makampuni ya simu ambayo yanaangalia maeneo kwa ajili ya uwekezaji ili yaweze kupata faida.
Aidha,Waziri Ndugulile amesema watu wote wanatambua kwamba mawasiliano kwa sasa sio anasa ni haki ya kimsingi ya kila mtanzania na kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote lengo kuu ni kuhakikisha kwamba wanapeleka mawasilino katika maeneo yote na kona zote za nchi
Amesema wamepiga hatua kama nchi ambapo amedai takribani asilimia 94 ya watanzanai wote wanapata mawasiliano ya njia ya moja ama nyingine.
“Kuanzia simu zetu za kitochi mpaka na wale wenye simu janja lakini Kijiografia asilimia 66 ya watanzania wanapata mawasiliano hii ni hatua kubwa naomba tujipongeze ninaposimama hapa tunakadi za simu ambazo zimesajiliwa milioni 52…..
“Na watu ambao wanatumia miamala ya simu wanaofanya miamala ya simu ni zaidi ya milioni 33 na simu kadi ambazo zimesajiliwa ambazo zinapata huduma ya internet ni zaidi ya milioni 29,”amesema.
Amesema wanapiga hatua na wana majukumu ya kuhakikisha wanafikisha mawasiliano ambapo kwa sasa wanataka katika simu za tochi waanze kutumia matumizi ya internet.
“Sisi kama Wizara kwanza tunamalengo makuu kupitia ilani ya CCM kutoka asilimia 43 ya matumizi ya internet hadi kufikia asilimia 80,”amesema
Amesema wanataka kuwekeze kwa kubadilisha Teknolojia ambapo 2G itaendelea kuwepo ambapo amedai sasa hivi dunia inaongelea 5G hivyo imeanza kuwaalika watu na makampuni ambayo yanaweza kuwekeza katika 5G.
“Tunataka kuamisha teknolojia hizi kwamba minara isiwe tu ya 2G bali iwe na uwezo wa matumizi ya 3G ambayo yanawezesha watanzania kutumia internet hata kule vijijini waweze kutumia internet tuna vijana wetu wamesoma wamejiari kule vijijini.
“Nilipata mrejesho wa kijana kule kijijini alinipigia simu ananiambia yeye yupo katika Wilaya mojawapo katika Mkoa wa Tabora ili aweze kupata huduma ya internet anahitaji kusafiri kilometa 128 sasa ni muhimu sana huko huko watu walipo tuweze kuwafikishia hizi huduma,”amesema
Amesema kazi nyingine ya mfuko wa mawasilino ni kuongeza huduma za mawasilino kwa njia ya redio ndio maana Wizara yake inasimamia na kutoa leseni za redio.
“Tunafanya kazi nyingine kubwa ya kukuza tehama na hivi karibuni tutakuwa na tukio la kuhakikisha shule zetu zinakuwa na Komputa ili waweze kusoma.Mfuko wa Mawasilino kwa wote unafanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha mawasilino ndani ya Nchi hayawi anasa bali yanakuwa ni haki ya msingi ya kila Mtanzania,”amesema
Amesema Serikali imesikiliza kilio cha watu wa pembezoni mwa nchi ambapo imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 45 ili mawasiliano yaweze kufika.
“Baadhi yenu mmekuwa mnasafiri mkifika kule mnapokelewa na Mawasiliano ya Nchi jirani sasa sisi kama Serikali tumedhamiria kuhakikisha tunaondokana na adha hiyo kwa kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alitamani kuona jambo hili tunalitekeleza
“Niseme jambo hilo na sisi tumelifanya tulituma timu zilienda zikazunguka mikoa yote ya pembezoni tumetangaza zabuni sasa hivi za zaidi ya shilingi bilioni 45 kwa lengo kuhakikisha mikoa ya pembezo ambako mawasiliano yanapokelewa na nchi jirani wanapata mawasilino vizuri,”amesema
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashimba amesema wanategemea kuanza maisha yao katika eneo la Ndejengwa ambapo amedai wameanza mradi Februari 15 2020 na mradi huo unategemea kukamilika ndani ya miezi saba.
Amesema wanategemea Novemba ofisi za jengo hilo ziwe zimekamilika ambapo Desemba watumishi wataanza kufanya kazi katika jengo hilo.
“Kwa kujenga jengo hili ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa awamu ya tano,Dk John Magufuli ambaye alisema taasisi za Serikali zihamie Dodoma na sisi tumefuata nyayo hiyo na tunaendelea kutekeleza katika awamu ya sita ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Amesema tunatemea katika eneo hilo watakuwa na sehemu la kufanyia michezo kama Soka na mingine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amesema ujenzi wa jengo hilo ni lazima uangalie watu wenye mahitaji maalum pamoja na matumizi ya tehama.
“Miaka hii ambayo leo teknolojia inakimbia kuliko mwaka Mheshimiwa Waziri ni vizuri tuendeleee ,kuwaelimisha wajenzi wapya wa majengo yanayotumika kwa umma wazingatie tehama.
“Hatutarajii miaka mitano tupate tena Waziri ambaye atakuwa anafunga mageti ili kuona watumishi waliochelewa kazini tunatarajia miaka mitano ijayo tusione tena Maafisa Utumishi anapiga mstari mwekundu chini ya kitabu cha watumishi ambao wamechelewa kuingia kazini,”amesema