Kesi Kuho Mfanyabiashara wa Tunduma amesema kitendo cha Mkuu wa Mkoa kuwatembelea ofisini wao watakuwa Mabalozi wa kuwashawishi wenzao ambao wamehamishia Biashara Nje kuzirudisha Nyumbani ili waweze kujenga Nchi.
Mkuu wa Mkoa amewatembelea baadhi ya wafanyabiashara kwa lengo la kupata uelewa wa sababu ya wafanyabiashara wa Tunduma kuhamia Nchi jirani pamoja na kustawisha Biashara za Tunduma.
“Ukiona watu wanahama ujue kuna tatizo na mimi nimeona nilijue Tatizo vizuri kwa kuwatembelea wafanyabiashara moja moja, kwani kuna baadhi wanashindwa kueeleza vizuri pale tunapokuwa tumeita mkutano wa pamoja” Omary Mgumba.
Kabanga Mpuyo muwakilishi wa Manyanya LTD amesema Kutokana na wafanyabiashara wa Tunduma kunufaika na faida ya uwepo wa mpaka wa Zambia na Tanzania pamoja na wakazi wa Tunduma kuingiliana kitamaduni na Mila wameiomba Serikali kuungalia Mji Tunduma kwa jicho la pekee kama vile, kutowasumbua wageni bila sababu wanapokuja Tunduma, kuondoa viziwizi vilivyowekwa kwenye baadhi ya Barabara unapoingia Tunduma kutokea Nchi jirani kwa tafsiri ya kuzuia Biashara ya magendo na Serikali kuzingatia umbali uliowekwa kisheria kwa wananchi wa Nchi jirani kuingia Nchi nyingine bila kuathiri Usalama wa Nchi.
Pia, wafanyabiashara wameomba elimu ya Kodi itolowe vizuri ili kuepuka kero ambazo zinazoweza kuzuilika.
Mkuu wa Mkoa Omary Mgumba amehaidi kuzitatua changamoto zote ambazo ni kero kwa ustawi wa Biashara kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Serikali.