Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara wa Viwanda na Biashara Bw. Dotto James, Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya wakipokea maelezo ya utendaji kazi wa maabara ya nguo na ngozi ya Shirika la Viwango Tanzania Leo Julai 08, 2021 alipofika kuzindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TBS leo Ubungo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara wa Viwanda na Biashara Bw. Dotto James, Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya wakipokea maelezo ya utendaji kazi wa maabara ya Maji na vimiminika ya Shirika la Viwango Tanzania Leo Julai 08, 2021 alipofika kuzindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TBS leo Ubungo Jijini Dar es salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara wa Viwanda na Biashara Bw. Dotto James, Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya wakipokea maelezo ya utendaji kazi wa maabara ya Chakula ya Shirika la Viwango Tanzania Leo Julai 08, 2021 alipofika kuzindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TBS leo Ubungo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango tanzania (TBS) leo Ubungo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Doto M. James akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango tanzania (TBS) leo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Dkt Fenella Mukangara akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango tanzania (TBS) leo Ubungo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akipata picha ya pamoja na Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo
**********************
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo amewataka Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania TBS kuongeza tija na thamani katika kutatua changamoto za msingi na kuhakikisha TBS inaendelea kuwa kwenye ubora wake.
Ameyasema hayo leo Julai 8,2021 wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, ambapo amewasisitizia kutambua majukumu yao ili wasiingiliane na majukumu ya Menejimenti.
“Nawakumbusha fanyeni majukumu yenu katika kutatua changamoto na sio kujiona kama waajiriwa wa TBS wakati ninyi ni wajumbe wa Bodi, shirikianeni kwa pamoja ili kutimiza malengo ya Taasisi”. Amesema Prof.Mkumbo
Amesema kuwa endapo Bodi itakuwa ni chanzo cha changamoto wataishauri serikali na kuivunja bodi hiyo, huku akisisitiza Bodi haiitaji mjumbe ambaye ni kikwazo katika kulipeleka shirika mbele zaidi.
Hali kadhalika Waziri Mkumbo ameikumbusha Bodi hiyo kuanza na viporo vilivyopo katika kutatua changamoto kwenye Taasisi ikiwemo pamoja na suala la ukaguzi wa magari bandarini na kuishauri manejimenti, lakini pia suala la wafanyabiashara wadogo kuona ni jinsi gani watatoa kwa urahisi alama za ubora kwa wafanyabiashara kwa kushirikiana na SIDO.
Naye Mwenyekiti wa Bodi Dkt Fenella Mukangara amehaidi kufanya kazi kwa bidii na kutatua changamoto zote na kuahidi kuwa msikivivu na kuishauri manenjimenti katika kujenga.