Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano naTeknolojia ya Habari,Dkt. Zainab Chaula akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizindua Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU).
Wadau wa elimu, sayansi na Teknolojia nchini wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akipata picha ya pamoja baadhi ya viongozi na wadau wa elimu, sayansi na Teknolojia nchini katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM.
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imesema imeanzisha vituo vya tamizi 17 ili kuhakikisha wanatatua changamoto mbalimbali zinazowakumba wabunifu wachanga nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sanyansi,Teknolojia na Ubunifu (STU) sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Tracer Study inayoangazia mchango wa ubunifu nchini.
Prof. Ndalichako amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa inawajengea ujuzi vijana ili ukawe manufaa kwa jamii inayowazunguka hivyo amewataka kutokata tamaa kwani wanashiriki katika kujenga nchi kwa bunifu zao zenye tija.
“Vijana wanahitaji kuaminiwa tunahitaji tuwape fursa, vijana wetu wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo tusiogope kuwakaribisha tuwape nafasi ili waweze kuonesha ujuzi wao”. Amesema Prof.Ndalichako.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu amesema wamekuwa wakiwafuatili vijana ambao wamepitia mafunzo ya ubunifu kwani lengo lao ni kuwasaidia wabunifu ili waweze kuonyesha mchango wao katika jamii.
“Kupitia ripoti hii aambayo imezinduliwa na kuweza kugaiwa kwa kila mmoja kikubwa kuangalia mchango wa ubunifu hapa nchini upi na kuweza kupata mrejesho kusudi tuweze kuboresha zaidi”. Amesema Dkt.Nungu.