Mkurugenzi wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo ya Yara Tanzania,Ruanda na Burundi , Winstone Odhiambo akizungumza katika uzinduzi huo wa Yara Connect uliofanyika mjini Arusha leo,(Happy Lazaro).
Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji na uzalishaji wa pembejeo za kilimo ya Yara Tanzania ,Ruanda na Burundi , Winstone Odhiambo akizungumza katika uzinduzi huo wa programu ya Yara connect uliofanyika mjini Arusha leo(Happy Lazaro)
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza katika uzinduzi wa programu ya mpango wa uaminifu wa malipo kwa wafanyabiashara wa rejareja wa Yara (Yara Connect) uliofanyika jijini Arusha leo.(Happy Lazaro).
********************************
Happy Lazaro, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mh.John Mongela amezindua programu ya mpango wa uaminifu wa malipo kwa wafanyabiashara wa rejareja wa Yara(Yara Connect) ambao utawawezesha wauzaji wadogowadogo wa bidhaa za Yara kuwasiliana kwa karibu na wakulima hususani walioko vijijini.
RC Mongela ameyasema hayo leo wakati akizindua programu hiyo katika mkutano uliowashirikisha wamiliki wa makampuni ya pembejeo za kilimo kutoka Arusha ,ambapo amesema programu hiyo itasaidia Sana kurahisisha huduma kutoka kwa wauzaji kwenda kwa wakulima ambao wengi wao wapo vijijini na wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji ufumbuzi wa haraka.
Amesema kuwa,serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika kampuni hiyo ili iendele kupanua wigo na kuwafikia wakulima zaidi ambao bado hawajafikiwa na huduma hiyo.
“Uzinduzi wa mtandao huu utasaidia Sana katika sekta ya kilimo kwani asilimia 58 ya wananchi wake hivi Sasa wanategemea kilimo kwani vyakula vyote vinapatikana kupitia kilimo , hivyo aliwataka wakulima kutumia mtandao huo kuwa nyenzo bora ya kuboresha kilimo chao ili kiwe na tija zaidi na mkulima kuweza kupata faida kubwa na kuweza kuzalisha zaidi .”amesema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Yara Tanzania ,Rwanda na Burundi inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji pembejeo za kilimo ,Winstone Odhiambo amesema kuwa,programu hiyo itasaidia Sana ufikishaji wa mbolea kwa wakati kwa wakulima hasa walioko maeneo ya vijijini.
Amesema kuwa,kupitia programu hiyo wakulima wataweza kupata elimu kupitia kwa wasambazaji wa mbolea kutoka Kampuni hiyo na kuweza kupata elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo bora na chenye tija.
“programu hii itatumika kwa wasambazaji wa mbolea ambapo wataweza kupata pointi kulingana na jinsi watakavyouza ambapo kupitia point hizo wataweza kupata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu,pikipiki na simu kulingana na pointi walizopata kupitia mauzo yao,hivyo programu hiyo ina faida kubwa sana kwani mbolea itakuwa inapatikana kila kijiji .”amesema .
Amesema kuwa,progamu hiyo ilishazinduliwa mkoani Kilimanjaro ,na Sasa hivi Arusha ambapo itazinduliwa mikoa Saba ya Tanzania ambapo amesema kuwa kampuni hiyo iko katika nchi 150 .
Kwa upande wake Mmiliki wa kampuni ya kusambaza pembejeo za kilimo ya Telemundo Agri Ltd,David Nyagah amesema kuwa, kupitia programu hiyo itasaidia sana kurahisisha huduma kati yao na wakulima hususani waliopo vijijini kwani wataweza kuitumia programu hiyo kutatua changamoto mbalimbali kwa kuwasiliana na kampuni ya Yara na kupata muafaka kwa haraka zaidi.