**************************
NA MWANDISHI WETU
Mhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya ICT-Kijitonyama Antony Elias ametengeneza mashine ya kutotoreshea vifaranga vya kuku (Incubator) ambayo inatumia biogas,LPG gas au gas asilia na kuweza kurahisha matumzi kwa mtumiaji.
Akizungumza na mwandishi wetu katika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam amesema Icubator hiyo haitegemei umeme pekee kufanya kazi kwahiyo hata umeme ukiwa umekatika inaendelea kufanya kazi kuongeza ufanisi katika utotoreshaji wa vifaranga vya kuku.
“Kwakua inatumia gas inasaidia utunzaji wa mazingira kwasababu ule uchafu watu wanautupa au wanatapisha vyoo kwasababu hawaoni manufaa yakeambapo pia unalipia lakini ukiwa na hii haiitaji tena kulipia kwasababu ule uchafu unakuwa tayari ni mali “. Amesema Mhandisi Elias.
Amesema utumiaji wa Biogas katika Icubator hiyo nikutafuta mtaalamu ambaye anaweza kutengeneza tanki ambalo utakuwa unalijaza samadi mbalimbali za wanyama kama ng’ombe. Kuku. na mabaki ya vyakula.