Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Nyasa bw Sikitiko Abdul akitoa pongezi kwa niaba ya wana CCM Wilaya ya Nyasa za Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi bora wa siku 100 na kumtaka aendelee na Moyo huwa wa kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.kikao hicho kimefanyika hivi karibuni katika ukumbi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Nyasa
…………………………………………………………
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nyasa Imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza Siku 100 kwa Uongozi wake imara.
Pongezi hizo, zimetolewa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilayani hapa, Bw. Sikitiko Abdul wakati wa kikao cha Baraza kuu la Umoja wa wazazi , uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za CCM zilizoko Mbamba bay Wilayani hapa.
Katibu Sikitiko amefafanua kuwa, Jumuiya hiyo inatoa Pongezi za Dhati kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hasani kwa Uongozi Makini na Imara aliouonyesha kwa Siku 100 za mwanzo tangu apokee Madaraka kutoka kwa Mtangulizi wake Hayati Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki dunia Tar 17.03.2021.
Ameongeza kuwa Mh Rais mpaka sasa amefanya mambo mengi na makubwa ya kuendelea, kutekeleza Miradi ya maendeleo ya kimkakati na kuhakikisha miradi iliyokuwa kwenye ilani ya chama cha Mapinduzi ya 2020 hadi 2025 inaendelea na kama ilivyo kwenye Kauli mbiu yake ya Serkali ya Awamu ya Sita inayosema “KAZI IENDELEE”.
“Jumuiya ya Wazazi CCM kupitia Baraza kuu lililoketi leo Tar 02.07 2021 linampongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Siku 100 za kuonyesha Uongozi Imara na kutekeleza miradi yote ya kimkakati Nchini ”. Alisema
Bw Sikitiko amesema kuwa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Nyasa inamshukuru sana Rais kwa Kutekeleza Miradi mikubwa ya Kimkakati Wilayani Nyasa ili kuwapa maendeleo wananchi na kuitaja miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa Barabara ya Mbinga Mbamba bay, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa, miundombinu ya Shule, Ujenzi wa Vituo vya Afya na miradi mingine mingi.
Jumuiya ya Wazazi CCM Wilayani Nyasa itaendelea kumuunga mkono kwa kuwahamasisha wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo na kufanya kazi kwa juhudi na m,aarifa ili kukuza kipato cha wananchi wilayani hapa kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
IMEANDALIWA NA
AFISA HABARI NYASA DC
0767417597.