Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Godfrey Mkamilo (kulia) kuhusu mche wa mti wa zabibu,alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo, iliyopo Makutopora Jijini Dodoma,leo Julai 5, 2021.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kitalu cha Shamba la zabibu alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), iliyopo Makutopora leo Julai 5, 2021 Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua na kujionea Shamba la Mkulima wa Zabibu Photunatus Kenyumko (katikati) lililopo Msalato leo Julai 5, 2021 Jijini Dodoma .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkulima Jully Sombe (kushoto), wakati alipotembelea shamba lake, lililopo Hombolo Jijini Dodoma, Julai 5, 2021
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia zabibu zilizovunwa kutoka kwenye shamba la mkulima, Stanley Swaga, wakati alipotembelea Shamba la mkulima huyo, lililopo Hombolo Leo Julai 5,2021 Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kuchakata zabibu cha CETAWIKO Florenzo Chesini, wakati alipotembelea kiwanda hicho ili kuona utendaji kazi wake, Hombolo leo Julai 5,2021 Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde wakati akiangalia skimu ya umwagiliaji ya mashamba ya wakulima wa zabibu iliyopo Hombolo jijini Dodoma leo Julai 5,2021.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
……………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imedhamiria kuliongeza zao la zabibu kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati ili kungeza thamani zao hilo na kuongeza tija kwa wakulima.
Amesema kuwa kampeni hiyo itaanzia mkoa wa Dodoma kwa kuwa imegundua kwamba zabibu ni fursa ya kiuchumi nchini na ardhi yote ya wilaya za mkoa wa Dodoma inakubali kilimo hicho.
Aidha Waziri Mkuu amezitaka taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ibadilike na kutoa mikopo kwa wakati.
Kwa upande wake Mkulima wa zabibu wa Chama cha Ushirika cha mradi wa umwagiliaji wa zabibu Wazamah July Sombe ameelezea changamoto walizonazo wakulima wa eneo hilo ni pamoja na miundombinu ya barabara kufika eneo hilo, ugumu wa upatikanaji wa mitaji kutokana na taratibu ndefu za mikopo za mataasisi ya kifedha, uchakavu wa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na riba kubwa ambazo ni vigumu kwa wakulima kumudu na kuendeleza kilimo hicho kwa uzalishaji mkubwa.
Aidha, mkulima huyo ameiomba Serikali kuimarisha masoko ya zao la zabibu kwa kuhamasisha wawekezaji zaidi kununua zao hilo ambalo bado upatikanaji wa soko ni changamoto.
Pia ameongeza kuwa kwasasa mkulima anazalisha tani 4-5 ya zabibu ambayo ni chini ya kiwango kinachoshauriwa na wataalamu cha Tani 15-20.