Home Mchanganyiko TMDA YATOA ELIMU KUHUSU MADHARA YA TUMBAKU KATIKA MAONESHO YA SABASABA

TMDA YATOA ELIMU KUHUSU MADHARA YA TUMBAKU KATIKA MAONESHO YA SABASABA

0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Bw. Adam Fimbo akizungumza katika katika banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Bw. Adam Fimbo akitika picha ya pamoja kwenye banda hilo na maofisa wa TMDA kulia ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma Bi. Gaudensia Simwanza na kutoka kushoto ni James Ndege Afisa Mawasiliano na Elimu kwa Umma na Robeta Feruz Afisa Mwasiliano na Elimu Kwa Umma 

Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma Bi. Gaudensia Simwanza akitoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea banda hilo kuhusu udhibiti wa matumizi ya Tumbaku.

Robeta Feruz Afisa Mwasiliano na Elimu Kwa Umma akiwapa elimu wananchi juu ya madhara ya utumiaji wa tumbaku kwenye maonesho ya  45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

James Ndege Afisa Mawasiliano na Elimu kwa Umma akizungumza na mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda hilo.

…………………………………………..

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA) imesema kuwa imejipanga kikamilifu kwa kujielekeza katika kutoaji wa elimu kwa wananchi juu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa Tumbaku.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Adam Fimbo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye  maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) ambapo ameeleza mikakati iliyopo ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku huku akitilia mkazo utoaji wa elimu kwa wananchi.

Ameeleza kuwa upo umuhimu wa kuwaelimisha wananchi juu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa tumbaku na kwamba anaamini kwa kuanza na elimu kutasaidia kuwafanya watu wengi ususani vijana kuacha kabisa matumizi ya tumbaku au bidhaa zinazotengenezwa na tumbaku.

“Jukumu letu la kwanza ni kuhakikisha kundi la vijana walio na umri chini ya miaka 18 hawahamasishwi au kushawishiwa kuingia katika matumizi ya tumbaku pia kuona ni jinsi gani wale ambao hawavuti sigara hawajiingizi kwenye uvutaji na wale ambao tayari wanatumia waache kwa kuanza taratibu mwisho waache kabisa” Amesema.

Ameongeza kuwa zipo sababu za msingi zinazowafanya kuelimisha jamii kuacha matumizi ya tumbaku ambazo ni pamoja na kuhepuka kupata magonjwa kama shinikizo la Damu na  mapafu kujaa maji huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo sehemu maalu za kuvutia sigara hasa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu.