*********************************
Na Silvia Mchuruza,
Bukoba,
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ametoa muda wa siku 7 kwa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, kutoa maelezo ya kwanini agizo la serikali la kutenga asilimia 40 ya makusanyo ya mapato ya ndani halikutekelezwa.
Akizungumza katika kikao maalum cha kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Kagera Rashid Mohamed Mwaimu katika taarifa ya CAG 2019/2020 kwa halmashauri hiyo lilisisitizwa suala la kutopelekwa kwa sehemu ya asilimia 40 ya mapato ya ndani yakiyokusanywa kwenye miradi ya maendeleo ambapo hoja hiyo ilibainisha kiasi cha shilingi milioni 256 .41 hazikupelekwa kwenye miradi ya maendeleo licha ya halmashauri kukusanya mapato ya ndani fedha zikiwa ni sehemu ya makusanyo halisi.
“Huo ni udhaifu mkubwa asilimia 40 inatakiwa iende kwenye mipango ya maendeleo ningependa nipate majibu ndani ya siku 7 kwanini hizo fedha hazikwenda katika ujenzi wa maendeleo” alisema Rashid Mwaimu.
Katika hatua nyingine Mwaimu ameitaka halmashauri hiyo kupata maelezo juu ya hatua gani zimechukuliwa kwa walio kusanya mapato zaidi ya shilingi milioni 22 na laki 8 na hazikwenda benki kwa mujibu wa Sheria za fedha za serikali za mitaa.
Mkuu huyo wa mkoa pia ameagiza kuwa wilaya zote ambazo hazikupeleka asilimia 40 ya mapato ya ndani kwenda kwenye miradi zitoe maelezo haraka sana ndani ya siku 7.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kyerwa Innocent Seba Bilakwate ameshauri miradi inayoanzishwa na halmashauri madiwani washirikishwe ili kuepuka fedha kupotea.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Bahati Henerico amepongeza juhudi za viongozi wa halmashauri hiyo zinazoiganya halmashauri hiyo kung’ara kwa kupata hati safi huku akiwataka madiwani hao kutunza siri za vikao na kuwajibika katika shughuli za maendeleo ili kuilete halshauri hiyo maendeleo.
Hata hivyo diwani wa kata ya Bugara Ferdinand Bishanga amese ili kuepuka madhaifu hayo fedha ikipatikana ipelekwe kwenye miradi husika kuliko kusababisha mrundikano wa fedha hizo.