Afisa Mwandamizi wa Forodha Chrisant Kyomushula (aliyeshika kifimbo) akimfafanulia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Suleiman Missango (wa pili kushoto) jinsi Kituo cha Pamoja cha Huduma Mpakani kinavyofanya kazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Suleiman Missango (wa kwanza kushoto) akipata maelezo katika banda la TRA kuhusu Idara ya Sera, Mipango na Utafiti
************************
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) Tanzania Dkt. Suleiman Missango ametembelea banda la TRA katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa na kuipongeza TRA kwa kujipanga vema kuwaelimisha na kutoa huduma kwa wananchi ambao wanatembelea maonesho hayo.
Pamoja na pongezi hizo ameishauri TRA kuendelea kutoa elimu ya kodi pamoja kuwafahamisha wanannchi huduma ambazo TRA inazitoa hususan huduma za kimtandao ili wananchi wengi zaidi waweze kuzielewa na kulipa kodi kwa urahisi.
“Nimefurahi kuona mmejiandaa vizuri kutoa elimu na huduma katika maonesho haya. Hongereni sana. Nafahamu mnatoa sana elimu lakini inabidi elimu hiyo iwe endelevu ili muweze kuwafikia wananchi wengi zaidi”, alisema Dkt. Missango ambaye aliongozana na baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya Tanzania (BoT).
Amesema kwamba kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wakurugenzi aliokuwa ameambatana nao kuna baadhi ya huduma zhawakuwa na ufahamu wa baadhi ya huduma zinazotolewa na TRA, inabidi kutoa elimu kwa kugawa makundi mbalimbali na kuwapatia elimu.
Amesisitiza umuhimu wa kuwaelewesha wananchi umuhimu wa kutumia tovuti ya TRA ambayo ina taarifa nyingi za masuala ya kodi na taratibu za kulipa kodi.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Elvida Max ambaye alimtembeza Mwenyekiti wa Bodi na ujumbe wake alimueleza kwamba, katika maonyesho haya ya 45 ya biashara ya Kiamataifa, TRA inatoa elimu kuhusu masuala ya mbalimbali ya kodi pamoja na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa walipakodi na kuwapatia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na huduma nyingine za kimtandao.
Dkt. Missango na ujumbe wake wamefurahishwa na huduma ya wafanyabiashara kutoa risiti bila kuwa na mashine ya efd, mfumo wa kubandika risiti a kielektroniki katika bidhaa pamoja na urahisi wa kusajili walipakodi kwa njia ya mtandao.
Katika Maonesho ya 45 ya biashara ya Kimataifa, TRA inatoa huduma ya kusajili na kuwapatia walikapkodi Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), kutoa taarifa ya makadirio ya kodi, maelezo ya matumizi ya mashine za EFD bila kuwa na mashine, jinsi mfumo wa ubandikaji Stempu za Kielektroniki katika bidhaa unavyofanya kazi pamoja na maelezo ya program za Chuo cha Kodi na jinsi ya kujiunga na chuo hicho.