WAZEE wa Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia wakati alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa bandari Kizimkazi, akiwa katika ziara yake.
WANANCHI wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza lka Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa bandari, akiwa katika ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea Chuo cha Mafunzo ya Amali Kisongo Makunduchi kuangalia maendeleo ya ujenzi huo akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, wakati wa ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyeklit Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mjasiriamali wa utengenezaji wa Tomato Ndg.Khamis Seif Ali (Kidume) wakati akitembelea mabanda ya maoneshi ya Wajasiriamali wa Wilaya ya Kusini Unguja akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Bi, Nasra Juma Mwalim wa Kikundi cha Shauri Moja cha Muyuni C Unguja, wakati akitembelea maonesho hayo ya Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini Unguja yaliofanyika katika viwanja vya mpira Paje.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiuliza mawasili wakati alipotembelea Kiwanda cha Mwani cha Furahia Wanawe Paje wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Watoto wa Kijiji cha Unguja Ukuu Kaebona baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kijiji hicho alipotembelea Tangi la Maji la Unguja Ukuu akiwa katika ziara yake Wilaya ya Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ( ZAWA) Dkt. Salha Mohammed Kassim, wakati wa ziara yake kukagua Tangi la Maji katika eneo la Unguja Ukuu Wilaya ya Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ziara yake kutembelea Tangi la Maji Safi linalotowa huduma ya maji kwa Vijiji vya Wilaya hiyo.
WANANCHI wa Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na Wananchi hao wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Wilaya hiyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Charawe baada ya kutembelea Kituo cha Afya cha Charawe akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja, na (Kulia kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Mhe.Rashid Hadidi Rashid.
WANANCHI wa Kijiji cha Charawe Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia baada ya kukitembelea Kituo cha Afya akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja.
(Picha na Ikulu