……………………………………………………………
Na Sixmund J.Begashe
Katika kuimarisha uwadilifu na uwajibikaji mahala pa kazi, Makumbusho ya Taifa imefanya mafunzo kuhusu mapambano na namna ya kuzuia rushwa kwa watumishi wake kama sehemu ya mikakati yake ya uboreshaji wa huduma.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika jiji Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema uadilifu, uaminifu na uwajibikaji ni sehemu muhimu katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa Tanzanaia.
Aidha Dkt Lwoga aliwaeleza wafanyakazi hao kuwa Taasisi imetekeleza na inaendelea kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuwajengea mazingira bora wafanyakazi wote hasa katika kuboresha maslahi yao na kuwapatia elimu ya utawala bora.
Akitoa mada ya “Nafasi ya wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa katika Mapambano dhidi ya Rushwa Mchunguzi Mkuu wa TAKUKURU, Mkoa wa Pwani Bw, Fredrick Mbigili amesema ni muhimu watumishi wa Taasisi hiyo kuwa waadilifu ili nchi iweze kunufaika na matokeo chanya ya kazi za kimakumbusho.
“Makumbusho ya Taifa inapokea wageni wengi, na wanahitaji huduma ya kutembezwa hatupendi kuona waongoza wageni wanadai Tip pia ni lazima kuwe na uwadilifu mkubwa kwenye zabuni mbali mbali pamoja na usimamizi wa miradi ya kimakumbusho” Alisisitiza Bw Mbigili
Bw. Mbingili ambaye pia ni Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma mkoa wa Pwani amesema suala la maadali kazini, Bw Mbili ni muhimu kwa mtumishi wa umma ajue misingi yake kutokakuwa na ubinafsi, kuwa mtiifu, kutokuwa na upendeleo, kuwajibikaji, kuwa mwaminifu na uongozi bora.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU tawi la Makumbusho Dar es Salaam Bwana Anastasius Liwewa, licha ya kuupongeza uongozi wa Mkumbusho ya Taifa kwa kuandaa semina ya Mapambano dhidi ya rushwa, amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka na kutoa wito kwa uongozi wa Taasisi hiyo kuendesha semina hizo mara kwa mara.
“Kwa niaba ya wafanyakazi wote, niseme tu kweli kuwa mafunzo haya yamezidi kutuimarisha sana kiutendaji, Mtoa mada ametufundisha kwa ustadi mkubwa kiasi sote tumemuelewa vizuri sana, tumeyachukuwa yote na tunaendelea kuyafanyia kazi kwa maslahi mapana ya Taasisi na nchi yetu kwa ujumla”. Alisema Bw Liwewa.
Mafunzo hayo ya Mapambano dhidi ya Rushwa yalitanguliwa na ufafanuzi wa maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyo yatoa siku ya Mei Mosi 2021 iliyofanyika kitafa Jijini Mwanza kuhusu maslahi ya wafanyakazi, uliotolewa na Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Makumbusho ya Taifa Bi Nuru Sovella.