Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Julai 4, 2021 amerejea nchini akitokea Paris nchini Ufaransa alikoshiriki Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makala pamoja na viongozi wengine wa ulinzi na usalama wa mkoa huo.