Mkurugenzi wa kampuni ya Baby Constable Limited Bi.Eva Michael akimpatiamtoto pakti ya coconut lishe mmoja wa watoto waliotembelea banda la kampuni hiyo leo katika Maonyesho ya 45 ya Kibiashara ya Kitaifa(Sabasaba) Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Baby Constable Limited Bi.Eva Michael akimpatia mmoja wa wateja pakti moja ya coconut lishe baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo leo katika Maonyesho ya 45 ya Kibiashara ya Kitaifa Jijini Dar es salaamMaonyesho ya 45 ya Kibiashara ya Kitaifa(Sabasaba) Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Baby Constable Limited Bi.Eva Michael akiwa na msaidizi wake wakitoa huduma kwenye banda la kampuni hiyo leo katika Maonyesho ya 45 ya Kibiashara ya Kitaifa(Sabasaba) Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Baby Constable Limited Bi.Eva Michael akiwa na msaidizi wake wakiwa tayari kutoa huduma kwenye banda la kampuni hiyo katika Maonyesho ya 45 ya Kibiashara ya Kitaifa(Sabasaba) Jijini Dar es salaam.
***********************
Kampuni ya kuzalisha Unga lishe ya Baby Constable Limited limewataka wananchi kwa ujumla kutembelea banda lao katika Maonyesho ya 45 ya Kibiashara ya Kitaifa(Sabasaba) Jijini Dar es salaam. na kuweza kujipatia unga safi kwaajili ya lishe ambao umeboreshwa zaidi.
Akizungumza na mwandishi wetu kwenye maonesho hayo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bi.Eva Michael amesema kuna umuhimu mkubwa kutumia unga wa Coconut lishe kwani inaimarisha afya na kuongeza uzito kwa watoto ndani ya muda mfupi pia inaongeza uzalishaji wa maziwa kwa wakina mama wanaonyonyesha.
“Mtoto yoyote ambaye hutumia unga huu huleta matokeo mazuri kwani una radha zuri pamoja na harufu inayovutia lakini pia kwa wakina mama wamekuwa wakitoa ushuhuda mzuri baada ya kutumia lishe hii”. Amesema Bi.Eva.
Aidha Bi.Eva amesema kuwa Coconut lishe pia unaweza kutumiwa na wakina baba ambao wanamajukumu makubwa kwani wengi wao wamekuwa na athari katika afya ya uzazi hivyo wengi walioweza kutumia lishe hiyo wameweza kuleta matokeo mazuri.
Unga huo unapatikana kwa ujazo tofautitofauti ambapo kilo moja inapatikana kwa shilingi 5,000 kwa rejereja na kuna boksi lenye katoni kilo 12 ambayo inapatikana kwa shilingi elfu 48.