Home Mchanganyiko WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT.DAMAS NDUMBARO AKIPONGEZA CHAMA CHA WASAFIRISHAJI WATALII...

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT.DAMAS NDUMBARO AKIPONGEZA CHAMA CHA WASAFIRISHAJI WATALII (TATO)

0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na  Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Wasafirishaji Watalii (TATO)  katika mkutano uliofanyika leo Jijini Arusha ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amekipongeza Chama hicho kwa jinsi kinavyoshirikiana na serikali katika kiutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta ya utalii.

**************************

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Damas Ndumbaro amevitaka Vyama vingine vyaUtalii nchini kuiga mfano wa  Chama cha Wasafirishaji Watalii ( TATO) kwa kuwa ni Chama bora cha Utalii nchini kwa jinsi kinavyojiendeshwa na kinavyojipanga wakati kinavyowasilisha hoja zake kwa Serikali kwa ajili ya maslahi mapana ya ustawi wa Utalii nchini

Amesema hayo leo Jijini Arusha wakati  wakati alipokuwa akizungumza na  Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Wasafrishaji Watalii (TATO) ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa luzungumza na Wadau wa Utalii nchini.

Amesema Chama hicho ni taasisi imara ambayo ipo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya utalii na sio vinginevyo.

Amesema Chama hicho kimekuwa kikijipambanua kwa kuhamasisha Wanachama wake kulipa kodi na tozo stahiki za Utalii ikiwa pamoja na kuishauri Serikali kuhusiana na kukuza na kuendeleza Utalii.

Amesema TATO imekuwa na rekodi nzuri hata pale inapotokea vyama vingie vya utalii vinapogoma kulipa baadhi ya tozo kwa ajili ya Utalii na kwenda mahakamani, Chama hicho kimekuwa hakiungani navyo kwa ajili ya maslahi ya mapana ya kuendeleza utalii.

Kufuatia rekodi hiyo, Waziri Dkt.Ndumbaro amewahakikishia Wajumbe wa Bodi wa Chama hicho kuwa ataendelea kushirikiana nao na atakuwa akitoa kipaumbele katika kuyashugulikia masuala yao.

” Ninaunda Kamati ya Ushauri ya masula ya Utalii ambayo ninyi kama TATO mtatoa Wajumbe watatu na Sisi Setikali tunatoa watu watatu kwa ajili  kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo tozo mbalimbali mnazozilamikia pamoja na suala la masoko.

Amesema kazi ya Kamati hiyo itakayoundwa itakuwa ikiishauri Serikali kea kufanya kazi kwa pamoja na Wizara yenye dhamana na Utalii kwa lengo la kukuza nakuendeleza sekta ya Utalii nchini

“Ninapokuwa na suala nyeti la Utalii nimekuwa nikiwashirikisha TATO kutokana na jinsi umakini wao na kujitoa kwao katika suala la utalii” alilisitiza Dkt.Ndumbaro

Amesema licha ya kuwa katika sekta yaUtalii  kuna vyama vya Utalii zaidi ya kumi lakini TATO imekuwa namba moja katika kutafuta suluhu za changamoto badala ya kuwa Walalamikaji kama vyamr vingine vilivyo.

Amesema tangu alivyoingia katika Wizara hiyo amejionea kuwa  chama cha TATO ni Chama chenye kilichojijengea heshima na hivyo kuwaahidi kuendeleza  ushirikiano na chama hicho.

 Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imesema ili uweze kuwwkeza katika Hifadhi ya Taifa  ya Serngeti ni lazima uwe Mwanachama wa TATO ili kuendelea kulinda hadhi na sifa ya Hifadhi hiyo Ulimwenguni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TATO, Willybroad Chamburo amemhakikishia Waziri Dkt. Ndumbaro kuwa katika Uongozi wake wataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa ajili aya maslahi mapana ya Sekta ya Utalii

Kati hatua nyingine, Mwenyekiti wa chama hicho, Chamburo amemshukuru Waziri huyo kwa kukubali kusitisha tozo ya uwekezaji ndani ya Hifadhi za Taifa kwa muda wa miezi mitatu iliyoanza kutumika Julai 1 mwaka huu.

Amesema kukubali kwake ni ishara tosha ya ushirikiano kati ya Chama hicho na Serikali katika kipindi kigumu cha changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19 ulioushambulia sekta ya Utalii duniani kote.